VIDEO-Makinda: Sio lazima ufikiwe leo, tuna siku saba kuhesabiwa

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda

Muktasari:

  • Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amewataka wananchi ambao hawatafikiwa na makarani wa Sensa leo kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa shughuli hiyo itaendelea kwa siku saba.

Dar es Salaam. Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amewataka wananchi ambao hawatafikiwa na makarani wa Sensa leo kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa shughuli hiyo itaendelea kwa siku saba.

Makinda amesema hayo jijini Dodoma baada ya Rais Samia Suhuhu Hassan kuhesabiwa kwenye Ikulu ya Chamwino Dodoma.

“Tumeanza leo, tutaendelea mpaka siku saba, makarani wakifanikiwa kwa leo watafanya kwa asilimia 15 tu. Tunaomba wananchi wasilalamike kama hawatafikiwa na makarani leo.” Amesema Makinda nakuongeza

“Sio lazima ufikiwe leo, ni siku saba. Tunaomba utulivu uwepo

Amewataka wananchi kuwa watulivu wakiandaa taarifa zao muhimu zikiwamo za Nida na mawasiliano ili kama karani hataelewa taarifa hizo atafanya mawasiliano.

Amesema sio lazima watu wote kukaa nyumbani kusubiria makarani hao.