Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO:Mwili wa Magufuli wazungushwa mara tano uwanjani, wananchi Dar waridhika

Mwili wa Magufuli wazungushwa mara tano uwanjani, wananchi Dar waridhika

Muktasari:

  • Baada ya shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kusitishwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza, mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe alitangaza utaratibu wa kuaga mwili kwa kuuzungusha uwanjani hapo.

Dar es Salaam. Baada ya shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kusitishwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza, mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe alitangaza utaratibu wa kuaga mwili kwa kuuzungusha uwanjani hapo.

Mwili huo ulipakiwa kwenye gari maalum lililokuwa na maofisa wa jeshi na kuzungushwa katika uwanja huo  mara tano ikiwa ni baada ya maelfu ya wananchi kuulizwa wanataka uzungushwe mara ngapi.

“Wananchi mwili utazunguka uwanja ukiwa kwenye gari mara tatu, kila mmoja pale alipo apunge mkono, tufanye kama bungeni wanaokubali  mara tatu waseme ndiyo,” amesema Gondwe lakini wananchi walikaa kimya.

Mkuu huyo wa Wilaya akauliza tena, “wanaosema hapana,” na wananchi wakajibu, “hapana” lakini aliposema mwili wa kiongozi huyo uzungushwe mara tano ili wamuage wananchi hao walisema kwa sauti, “ndio.”

Kuanzia saa 9:23 alasiri gari lenye mwili huo lilianza kuzunguka uwanja huo huku mamia ya wananchi wakipunga mkono na wengi kuonekana wakifuta machozi. Msafara ulizunguka uwanja huo hadi saa 10:10 jioni na kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya safari ya Dodoma.