Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Samia ataja changamoto zinazokwaza amani Afrika

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani la Usalama la Umoja wa Afrika, unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024. Picha na Sunday George

Muktasari:

  •  Wakati Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika likitimiza miaka 20 tangu kuanzishwa, Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, amesema bara hilo bado linakabiliwa na tishio la ugaidi na mabadilishano ya Serikali bila kufuata katiba.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameutaja ugaidi unaoletwa na imani kali, mabadiliko ya Serikali yasiyofuata katiba, yasiyozingatia utawala wa kiraia kuwa matisho ya usalama yanayoikabili Afrika. 

Rais Samia ameyasema hayo leo Mei 25, 2024 alipokuwa akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC) unaofanyia jijini Dar es Salaam.

Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo, amesema licha ya mafanikio ndani ya miaka 20, bado bara la Afrika limeshindwa kunyamazisha kelele za mtutu wa bunduki kutokana na migogoro na uhalifu wa madaraka unaoendelea.

“Tumeshuhudia migogoro, uhalifu wa madaraka na kutokuwepo kwa juhudi za kudhibiti. Katika yote, bado hatujaweza kunyamazisha mtutu wa bunduki Afrika,” amesema.

Samia ametaka kutekelezwa kwa maelekezo ya vikao vya wakuu wa nchi za Afrika katika kupambana na matishio hayo.

“Masuala mawili yanayotishia amani ni ugaidi na imani kali inayosambaa maeneo yote ya Afrika.”

“Tishio la pili ni kuwepo kwa mabadiliko ya Serikali bila kufuata katika, tunapaswa kujiuliza kwa nini tunarejea tena huko?

“Kuendelea kwa changamoto hizo kunaibua maswali ya msingi, kwa nini yanaendelea? Je, tunatumia maadili yetu vizuri kukabiliana na masuala haya?” amehoji huku akitaka mkutano upo uwe na majibu.

Ili kukabilia na changamoto hizo, amependekeza hatua za kuchukuliwa ikiwa pamoja na kuzuia migogoro inayoendelea kwa majadiliano na maridhiano.

“Katika nyezo za umoja wa Afrika tunayo mifumo ambayo haitumiki vizuri kwa sasa, hivyo naamini utekelezaji madhubuti wa nyenzo hizo ukiwa pamoja na mipango ya kunyamazisha mitutu Afrika ni muhimu katika kuimarisha amani na usalama. 

“Ni muhimu pia kutumia jeshi la utayari la Afrika na mfuko wa amani wa Afrika kuongeza uwezo wa kutekeleza mipango yetu ya usalama,” amesema.

LIVE: Rais Samia, vigogo wa Afrika washiriki maadhimisho ya miaka 20 PSC

Kuhusu ushirikiano wetu na wadau, ameutaka umoja huo kuwashirikisha wanawake na vijana katika michakato ya amani.

“Kidunia tunatakiwa kuongeza ushirikiano na wadau wakiwamo Umoja wa Mataifa, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), asasi za kiraia na wengineo,” amesema. 

Huku akinukuu kauli ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela inayosema: ‘Amani ni kutengeneza mazingira ambayo kila mtu anaweza kustawi,’ .

Samia ametaka kuwepo kwa jitihada za pamoja katika kukabiliana na changamoto za kiusalama na kukuza maendeleo ya kijamii.

Kuhusu mafanikio, Rais Samia amesema tangu baraza hilo lilipoanzishwa miaka 20 iliyopita, kumekuwa na jitihada za kuanzisha majadiliano ya upatanishi hadi kusaidia nchi kujengwa upya baada ya vita.

“Baraza limekuwa na mchango katika kukabiliana na migogoro na matisho ya usalama, kutoka Sahel hadi Somalia. Baraza pia limechangia juhudi za bara letu kukabiliana na ugaidi,” amesema.

Pia amesema baraza hilo limejizatiti kusimamia misingi ya haki za binadamu, demokrasia na utawala bora, na ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika amani na usalama.

“Katika ngazi za Taifa, baraza limeshirikiana na nchi zinazokabiliwa na usalama na kufanya ziara katika nchi hizo ambazo  zimeliwezesha baraza kuelewa vema changamoto za usalama, kusikiliza kwa wanaohusika na wanaoathiriwa na migogoro hiyo.

“Kikanda, baraza linaendelea kushirikiana na jumuiya za uchumi za kikanda ili kuimarisha utaratibu wa jitihada za amani na usalama na kubadilishana uzoefu.

“Baraza limekuwa na ushirikaiano wa kitaasisi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kamati ya siasa na usalama ya Umoja wa Ulaya na kuongeza ushawishi wa bara la Afrika duniani,” amesema.