Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makamba aeleza mchango wa Tanzania kulinda amani Afrika

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa wa Tanzania na wa Afrika Mashariki ukiimbwa kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024.

Muktasari:

  •  Makamba ametaja mchango wa Tanzania katika kulinda amani ya Afrika kuwa ni pamoja na kuchangia vikosi vya kulinda amani kwenye Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, pamoja na misheni ya pamoja ya Afrika na Umoja wa Mataifa kule Liberia (ECOMOG).

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ameeleza mchango wa Tanzania katika kulinda amani na usalama barani Afrika, akisema imeendelea kuuenzi msimamo wa Rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Nyerere.

Makamba ameyasema hayo leo Mei 25, 2024 katika maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Usalama na Amani la Afrika (PSC) jijini Dar es Salaam linalohudhuriwa na marais wastaafu, viongozi wa majeshi, Umoja wa Afrika na mgeni rasmi akiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tangu awali, Tanzania chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, ilionyesha mchango wa kuwa na Afrika yenye amani. Tanzania ilikuwa sekretarieti ya ukombozi wa Baraza la Usalama la Afrika.”

“Tulisema uhuru wa Tanzania hautakuwa kamili bila kuwa na uhuru wa bara zima la Afrika,”amesema Makamba.

Ametaja mchango wa Tanzania katika hilo  ni pamoja na kuchangia vikosi vya kulinda amani kwenye Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, pamoja na misheni ya pamoja ya Afrika na ile Umoja wa Mataifa kule Liberia (ECOMOG).

LIVE: Rais Samia, vigogo wa Afrika washiriki maadhimisho ya miaka 20 PSC

Pia ametaja vikosi vya Tanzania vilivyo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) vilivyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji.