Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SADC yaitisha mkutano wa dharura

New Content Item (2)

Muktasari:

  • Wakuu wa Nchi za SADC kukutana kwa dharura Angola kujadili juhudi katika kuinarisha hali ya amani, ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Dar es Salaam. Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) wanatarajia kukutana katika mkutano wa dharura jijini Luanda, Angola kesho Novemba 4, 2023.

Mkutano huo unalenga kujadili juhudi za Sadc katika kuimarisha hali ya amani, ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufuatia mapigano ya muda mrefu yanayoendelea nchini humo yakitekelezwa na vikundi vyenye silaha katika majimbo ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri.

Mei, 2023 mwaka huu Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walikutana jijini Windhoek nchini Namibia nakuridhia nchi za SADC kuunga mkono Serikali ya DRC na kushughulikia hali ya usalama ya Mashariki mwa nchi hiyo kabla ya uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Novemba 3,2023 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali imeeleza kuwa katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania unatarajiwa kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba na maaofisa waandamizi wa Serikali.

Pamoja na masuala mengine, mkutano huo unatarajiwa kusisitiza umuhimu wa utashi wa kisiasa kwa nchi wanachama katika kuchangia askari na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya Misheni ya Ulinzi wa Amani ya Sadc nchini DRC (SAMIDRC), ambapo hadi sasa nchi tatu pekee ndizo zimechangia askari na vifaa vya kijeshi katika misheni hiyo.

Katika taarifa hiyo wamezitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Afrika ya Kusini pamoja na Malawi.

Mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama na kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu na Mawaziri vitakavyofanyika Novemba 3 mwaka huu.