Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Vilio vyatawala Mchungaji Kantante, mzee wa kanisa wakiagwa

Majeneza yenye miili ya Mchungaji Kantate Munis ambaye alikuwa mchungaji Kiongozi wa usharika wa Kimashuku Jimbo la Hai la Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la KKKT na Mzee Laban Kweka ambaye alikuwa Mzee wa Kanisa hilo, ikiwa katika Kanisa la Eben-Ezer usharika wa Kimashuku kwa ajili ya Ibada ya kuagwa kwa miili hiyo. Picha na Omben Daniel

Muktasari:

  • Mchungaji Kantate Munis (42) anatarajiwa kuzikwa kijiji kwao Kisamo Old Moshi kesho Ijumaa. Kiongozi huyo alifariki katika ajali pamoja na mzee wake wa usharika, Laban Kweka (50) ambaye atazikwa leo.

Hai. Mamia ya waombolezaji wakiongozwa na jopo la wachungaji kutoka Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefurika nje na ndani ya Kanisa la Ebenezer Usharika wa Kimashuku wa Kanisa hilo wilayani hapa kwa ajili ya kuaga miili ya mchungaji Kantate Munis (42) na mzee wa kanisa, Laban Kweka (50).

Vilio vyatawala mchungaji, mzee wa kanisa wakiagwa

Wakati miili hiyo ikiagwa kanisani hapo, vilio na simanzi vimetawala kwa waombolezaji waliofika kwa ajili ya kushiriki ibada hiyo, huku wengine wakishindwa kujizuia na kuanguka.

Msaidizi wa Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati la Dayosisi ya Kaskazini, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Israel Moshi mbaye ni mume wa Mchungaji Kantate Munis, akiwa na watoto wake wanne, wakati wa ibada ya kuaga miili ya Mchungaji Munis na Mzee Laban Kweka. Picha na Omben Daniel

 Mwili wa Mzee wa kanisa hilo, utazikwa leo Agosti 8, 2024 kwenye makaburi ya familia eneo la Kimashuku Wilaya ya Hai, huku mwili wa mchungaji Katante ukisafirishwa kupelekwa kijijini Kisamo Old Moshi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika kesho Ijumaa Agosti 9, 2024.

Mchungaji Munisi ambaye alikuwa mchungaji kiongozi wa usharika wa Kimashuku, pamoja na Mzee Laban Kweka (50) walifariki dunia kwa ajali Agosti 4, 2024 baada ya gari walilokuwa wakisafiria wakitokea kwenye uimbaji wa Kanda Usharika wa Gezaulole wilayani Hai, kugongwa na basi la Shabiby.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na usharika huo, inaeleza kuwa, Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Fredrick Shoo ataongoza mamia ya waombolezaji kesho Ijumaa, Agosti 9 kwenye maziko ya Mchungaji Kantate ambaye atazikwa Kisamo.

Tarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro juzi Agosti 6, 2024 Simon Maigwa ilisema ajali hiyo ilitokea Jumapili Agosti 4, 2024 katika eneo la Kimashuku, Kata ya Mnadani Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Aidha, Kamanda Maigwa alisema dereva wa Basi hilo amekamatwa kwa taratibu za kisheria kwa kuwa alifanya uzembe kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.