Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 10,000 waliopata mimba za utotoni, shuleni kupewa mafunzo

Afisa Programu wa Kitaifa, Ubalozi wa Uswiz, Rasheed Mbalamula akizungumza Septemba 26, 2023 wakati wa uzinduzi wa kutambulisha tamasha la Ujuzi kwa Vijana yanayotarajiwa kufanyika kwenye Wilaya za Mvomero, Kilosa, Gairo, Malinyi, Mlimba (Kilombero) pamoja na Manispaa ya Morogoro. Picha naLilian Lucas.

Muktasari:

  • Katika kuhakikisha Vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wanafikiwa Ubalozi wa Uswisi na mtandao wa Mviwamoro umelenga kufanya tamasha lenye tija kwa kuwapatia ujuzi wa stadi.

Morogoro. Vijana 1,600 kutoka halmashauri sita za Mkoa wa Morogoro kushiriki  bonanza la ujuzi lenye nia ya kuwajengea uwezo katika ufundi stadi pamoja na kilimo huku vijana 10,000 wengine kufikiwa mwakani.

Bonanza hilo limeandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji mkoa wa Morogoro (Mviwamoro) kwa kushirikiana na

Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania.

Ofisa Programu wa Kitaifa, Ubalozi wa Uswisi, Rasheed Mbalamula amesema hayo Septemba 26, 2023 wakati wa uzinduzi wa kutambulisha matamasha hayo yanayotarajiwa kufanyika kwenye Wilaya za Mvomero, Kilosa, Gairo, Malinyi, Mlimba (Kilombero) pamoja na Manispaa ya Morogoro.

Aidha Mbalamula amesema vijana hao 1,600 watafikiwa ndani kwa miezi mitatu kupitia bonanza huku kila wilaya ikitoa vijana 200 na  vijana 600 kwenye bonanza kubwa litakalofanyika Manispaa ya Morogoro.

Amesema tamasha hayo ni mwendelezo miradi miwili, mradi wa Skills for Employment Tanzania (SET) unaotekelezwa na Swisscontact pamoja na mradi wa Oppotunity for Youth Employment (OYE) ambayo inafadhiliwa Serikali ya Uswisi.

Paul Mideye mtaalamu wa vijana kutoka Swisscontact, amesema mradi  SET unatarajia  kuwajengea uwezo vijana 10,000 kwa mwaka 2022 hadi mwaka 2926, kati yao 1,000 ni wale waliopata mimba wakiwa watoto au shuleni.

"SET unaolenga vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kwa kuwajengea uwezo katika ufundi stadi hususani katika kilimo nia ni kuwawezesha ili waweze kujitegemea,"amesema.

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wamefanikiwa kuwafikia vijana 2,600 ambapo mradi utaendelea kutekelezwa hadi mwaka 2026 kwa kutawafikia vijana hao 10,000.

Amesema changamoto walizokutana nazo ni pamoja na vijana hao kutokuwa na mitaji hivyo kushindwa kutekeleza kile walichofundishwa na nikutokana na wengi wao kuwa na umri mdogo kwa maana chini ya miaka 18.

Kwa upande wake Bonnitha Gahaiha Mshauri wa ujuzi wa vijana na Jinsia kutoka Mradi wa OYE amesema mradi  huo unalengo la kufikia vijana 4,250 wenye umri wa miaka 18-30 walio nje ya mfumo rasmi wa elimu, waishio vijijini na maeneo yalio pembezoni ya miji.

"Hadi sasa tumefanikiwa kufikia vijana 4,393 sawa na 103% ambao wamepata mafunzo ya ufundi stadi, biashara, na stadi za maisha kupiti mfumo usio rasmi na kujiunga katika vikundi vinavyojishughulisha na shughuili mbalimbali za kiuchumi." amesema.