Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana wakulima watakiwa kupata ujuzi wa ufundi stadi

Muktasari:

  • Ujuzi kwa vijana utatengeneza ajira kupitia elimu ya ufundi stadi ambao ndio njia pekee ya mafanikio kwa kujipatia kipato na kuweza kutatua changamoto.

Mlimba. Vijana wanaofanya shughuli za uzalishaji hasa kilimo na ufugaji, wamehimizwa kujikita kwenye ujuzi wa stadi za ufundi kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao kwa sababu ufundi ni mtaji wa muda mrefu usioisha thamani.

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi Wakulima na Wafugaji Morogoro (Mviwamoro) Selemani Balali alisema hayo Oktoba 10,2023 katika uwanja wa Matangini, Halmashauri ya Mlimba wilayani Kilombero kwenye maadhimisho maalum ya kuwahimiza vijana kutumia ufundi stadi na kilimo ili ajili ya kujiajiri yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Uswiss nchini Tanzania.

Balali amesema vikundi vya vijana vingi vimeweza kunufaika kutokana na kilimo na ufugaji na kuwafanya kuweza kujiajiri na kuajiri wengine.

“Mafunzo yanayohusiana na kilimo vijana yamewanufaisha na sasa ivi wameshakuwa na mitaji yao wenyewe na kuweza kupanga bei kwa mazao wanayolima na kuna vikundi vichache si wote wamaenufaika hasa wale waliokata tamaa hawataki kujishughulisha naeza kusema ni uvivu tu, lakini bado tunaendelea uhamasisha ili wajiamini," amesema.

Afisa Mtendaji wa Kata Mlimba, Wolfram Mhiche amesema mafunzo ya ufundi stadi yamekuwa yakisaidia kwa kiasi kikubwa vijana hususani wa maeneo ya mijini kutokana na wingi na kuwepo kwa fursa nyingi, huku akiwataka vijana walioko pembezoni kwa maana ya vijijini kutokana tamaa.

Kijana mnufaika wa Kijiji cha Msolwa, Charles Ngagaya yeye amejifunza kilimo hai kisichotumia mbolea ya kisasa na badala yake wamekuwa wakitumia mbolea asili kama kinyesi cha ng’ombe na mbuzi.

“Kikundi chetu tayari tuna shamba la mboga ila natoa hamasa kwa vijana wenzangu kuendelea kujiweka sawa kwenye shughuli za uzalishaji mali,”amesema.

Mratibu wa Mafunzo ya Vijana, Mradi wa Skills for Employment Tanzania (SET) na Opportunity for Youth Employment (OYE) inayofadhiliwa na Serikali ya Uswisi, Victoria Nkuba amesema matarajio ni vijana kuweza kuinuka zadi kiuchumi kwa kuyafanyia kazi na kuwaongezea kipato.

“Vijana lazima waongeze nafasi ya kujiajiri na kuachana na fikra za kutegemea kuajiriwa,” amesema.

Mtaribu wa Mviwamoro ambao ni waandaaji wa Tamasha la Kaa Kijanja, Ufundi Stadi, Ajira kwa Vijana, Joseph Sengasenga amesema walengwa ni vijana ambao ni wazalishaji wanaofanya shughuli za uzalishaji hasa kilimo na ufugaji hivyo kama Mviwamoro katika halmashauri nyingine watafanya maeneo ambayo vijana husika watafikiwa.

Sengasenga amesema wanaendelea kuelimisha na kuhamasisha hasa katika kuwajengea uwezo kiujuzi na kuongeza thamani hasa kwenye bidhaa zao na kuweza kufanya shughuli nje ya kilimo.