Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa CCM watakiwa kutumia ofisi zao kutatua kero za wananchi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa CCM jimbo la Isimani.

Muktasari:

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas amewataka viongozi wa chama hicho kutumia Ofisi zao kama sehemu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Iringa. Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kutumia ofisi zao kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Wito huo umetolewa leo Mei 20, 2024 na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa CCM katika jimbo la Isimani.

Asas amesema ni ajabu kuona kijiji, tawi au kata wananchi wana manung'uniko, Serikali ya eneo husika haijawasikiliza na chama kinashindwa kutoa sauti kwa ajili yao.

Mnec huyo ameanza kutekeleza ahadi yake ya kujenga ofisi za CCM kwenye kila kata akianzia na jimbo la Isimani linaloongozwa na mbunge wake, William Lukuvi.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Jimbo la Isimani kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Asas amesema viongozi wa chama hicho wanapaswa kuwa wa kwanza kutatua changamoto za wananchi.

“Kuna kata ya Isimani Ofisi haijaanza kujengwa? Nimeanza na Isimani kumpa shukrani Mh Lukuvi lakini sasa ofisi hizo zikawe sehemu ya kutatua kero ya wananchi. CCM iwe kimbilio lao,” amesema Asas.

Amesema zamani watu wengi walikuwa wakikimbilia ofisi za CCM kuelezea shida zao ikiwamo matatizo ya kijamii kama ndoa.

Asas amewashauri viongozi wa CCM kuwapitisha viongozi wanaokubalika kwenye jamii katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

“Tuleteeni wagombea ambao wanapendwa na wananchi, wale waliokubalika, walio madarakani sasa angalieni kama wanafanya kazi za wananchi,” amesema Asas.

Kwa upande wake, Mbunge wa Isimani, William Lukuvi amesema anao uhakika kwamba hakuna kijiji ambacho kitaenda upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kazi zinazoendelea kufanyika.

“Kila kijiji kina maendeleo yamefanyika, kama sio maji, huduma za afya, elimu, barabara na mengine mengi. Wananchi wanaona na siyo sisi viongozi tu,” amesema na kuongeza:

“Tupendane, tushikamane na tufanye kazi za chama kwa undugu, sisi ni ndugu.”

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Costantino Kihwele amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye jimbo hilo unaendelea vizuri.