Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa dini wataka wananchi wasikilizwe kero zao

Waumini wa Kikristo wakiwa kanisani. Picha ya Maktaba

Muktasari:

Ni kauli zilizotolewa wakaati wa mkesha wa Krismas

Dar es Salaam. Umeme wa uhakika, barabara zinazopitika, kodi rafiki kwa wananchi, huduma bora za afya, elimu na mazingira bora ya kazi, ni kero kwa wananchi zilizotajwa na viongozi wa dini wakitaka Serikali izifanyie kazi.

‘’Habari njema na furaha wanayoitaraji wananchi ni uchumi mzuri unaoleta maendeleo katika nyanja zote, miundombinu bora, barabara zinazopitika wakati wote, lakini pia habari njema kwa wananchi ni pale ambapo tutakuwa na umeme wa uhakika, huduma bora za afya, elimu na mazingira mazuri ya kufanya kazi,


Pia habari njema kwetu wananchi ni kodi rafiki inayowawezesha wafanyabiashara kuendeleza biashara zao vizuri,” ni kauli ya Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Geita, Reuben Ng'wala katika Ibada ya mkesha wa Krimas Kitaifa katika Kanisa la AICT Yeriko Dayosisi ya Geita.


Akinukuu kitabu cha Luka 2-10 kuhusu habari njema, Askofu Ng’wala alisema hakuna mtu anayependa habari mbaya, akisisitiza habari njema ambayo ni faraja kuu kwa Watanzania ni wokovu unaopatikana kwa kumwamini Yesu Kristo ili kupata haki, amani, baraka, upatanisho na uzima wa milele,

Jambo lingine alilosisitiza Askofu Ngwala, habari njema kwa Watanzania ni pale kutakapokoma unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, mauaji, ufisaji na ujambazi.

“Kwetu Geita mauaji yanakuwa makubwa sehemu za mialo na machimbo, vifo vinakuwa vingi na namshukuru Mungu ajali zinapungua. Pia kwa watu wa Mkoa wa Geita habari njema ni kukamilika kwa daraja la Kigongo Busisi ambalo litaondoa kero nyingi za kukaa feri kwa muda mrefu na kupoteza muda mwingi,” alisema.


Mbali na hayo, Askofu Ng’wala alisema habari njema kwa wananchi wa Geita ni pale watakapokuwa na na stendi bora na kubwa ya mabasi ya mkoa ili wanapofika wafurahie huduma nzuri.


Wajibu wa wananchi

Akizungumzia wajibu wa wananchi kwa Serikali, Askofu Ng’wala alisema habari njema haikomei kwa wananchi tu, kwa kuwa haki huambatana na wajibu,


“Habari njema kwa Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi, habari njema na furaha kwao ni kuona watu wote kwa dini zao wanaiombea Serikali kwa majukumu yake makubwa na mazito ya kulinda utulivu amani, mshikamano na usalama wa nchi nzima,


Aliongeza: “Kwa hiyo habari njema na ya furaha kuu kwa Serikali yetu, ni kuona tunaiombea ili itimize yale mambo iliyopanga kufanya katika nchi ya Tanzania, lingine ni kuona wananchi wote wanafanya kazi kwa bidii na weledi wakiunga mkono juhudi za Serikali kwa uaminifu,”amesema.


Alisema Serikali chini ya Rais Samia inafanya mambo makubwa hivyo ili iendelee kutekeleza mambo hayo ni wajibu wa wananchi kuiunga mkono Serikali katika juhudi zake kujenga hospitali, shule, zahanati.

Mbali na hayo, Askofu Ng’wala alisema habari njema ya furaha kuu ni wananchi wanapotii sheria bila shuruti akisistiza ni wajibu wa Wakristo kuwa kielelezo kutii mambo yanayoelekezwa na viongozi na watawala kwani ndio itakuwa habari njema.

Katika Ibada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella alisema Serikali chini ya Rais Samia inatambua mchango wa madhebebu ya dini katika amani na utulivu uliopo nchini.

“Bila amani na utulivu na mshikamano huu mkusanyiko usingekuwepo, endeleeni kumuomba Mungu aiweke Tanzania katika Amani na utulivu,Rais samia ana dhamira ya dhati na mkoa wa Geita na Watanzania ndio maana alipoingia madarakani amekuwa akihubiri upendo na maridhiano ili Watanzania wote kujiona ni sehemu ya Serikali,”alieleza.


 Kuhusu uchaguzi na amani

Katika hatua nyingine, Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Jackson Sothtenes, akitoa salamu za sikukuu Krismas,  aliwataka  wananchi kuachana na dhana potofu ya siasa ni mchezo mchafu kwani  kuamini hivyo  ni kubariki kuwa na viongozi wachafu.

Alisema mwakani kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwaka uaofuata uchaguzi mkuu hivyo waepuke kuchagua viongozi wanaotoa kwa endapo watawachagua watakuwa wakiongozwa na wakaowaibia kwa miaka yote mitano.

"Niwaombe sana wananchi, chaguzi unakuja kila mtu ashiriki kwa vile atakavyoweza, iwe kuchagua au kuchaguliwa kwa kuwa kikatiba ni haki yako.

"Kama kanisa tunaombea uchaguzi ukafanyike kwa haki na amani ili Taifa letu lisimame imara kwa kuwa uchaguzi ni kitu kinachopita lakini amani ya Tanzania ni bora zaidi kuliko itikadi ya chama au au mtu mmojammoja,"alisema.

Askofu Sothtenes alisema ili Tanzania iendelee kudumu na amani, ni vema kuepukwe siasa za chuki na watu kukumbuka Tanzania ina thamani kuliko mtu mmoja na maisha ya Watanzania ni ya vizazi kwa vizazi.


Naye Joram Haule,mkazi wa Sinza aliyeshiriki ibada hiyo alisema suala la watu kushiriki uchaguzi elimu ya uraia inatakiwa kuendelea kutolewa ikiwemo mashuleni ili kuwajenga viongozi wajao.

Msisitizo wa kudumisha amani unaungwa mkono na Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh ambaye aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu ya Krismasi wakijiepusha na migogoro, fujo na malumbano.

“Kila mmoja amuheshimu mwenzake bila kujali kipato chake wala dini,vitabu vya Mungu vinataka kuwa na amani, furaha na upendo na hakuna anayetaka fujo na malumbano,”alisema.

Mbali na hayo Askofu Hafidh aliwataka vijana kutokubali kushawishika kuingiza kwenye makundi ya watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya pamoja na kushiriki vitendo vya udhalilishaji.

“Vijana wanadanganywa kuingia kwenye vitendo hivi, kwahiyo wanatakiwa wajijue wana malengo gani kwani taifa linapoteza rasilimali na nguvu za taifa kutokana na vitendo hivyo,” alisema


Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Zanzibar International Christian Center (ZICC), Dickson Kaganga alisema: “Tusherekee kwa utukufu wa Mungu hakuna jambo linaumiza watu kupata majanga na ndoa kuvunjika kwasababu ya krisimasi hivyo ni vyema kulikumbuka hilo na watu kujitahidi kuwasaidia wenye mahitaji.”

Kwa upande wake, Mchungaji Shukuru Stiven Maloda wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Zanzibar, aliwataka waumini kuwaombea waliopo kwenye changamoto za kivita ikiwemo eneo ambalo Yesu alizaliwa Israel, akisema hawawezi kusherehekea kwasababu ya migogoro ya kivita.

“Tufurahi sikukuu hii kwa amani na kwa pamoja, isiwe sikuku ya fujo na mafarakano, tusihau kua wa amani na utulivu ndio tunu za taifa letu tunatakiwa kuvitunza,” alisema

Aliwaomba wananchi kujitokeze kujiandikisha na kupiga kura bila kusababisha uvunjifu wa amani katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.


Kukataa dhambi, tamaa

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki ya Pwani Azania Front lililopo Dar es Salaam, Alex Malasusa amesema leo sio maadhimisho tu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Kristo bali tunatukumbushwa kuwa ni lazima Yesu azaliwe katika maisha yetu, hivyo lazima tuende kwa njia ya Mungu.

Katika hilo amesema haina budi kuacha dhambi, tamaa, hivyo watu wanapaswa kukumbatia haki na utauwa.

"Mungu anatupenda lazima twende kwake kwa faida. Neema ya kuzaliwa kwake ni ya kwetu sote hivyo lazima tuukatae ubaya na tamaa za kidunia," amesisistiza.

Katika kukazia hilo Askofu Malasusa amesema kuna watu wanatamani kufanikiwa na kuwa matajri kwa siku moja, amesema neema inakataa hilo hivyo kuzaliwa kwa Yesu kutawaondoa katika tamaa za kidunia.

"Ishi kwa kiasi kuna watu hawana kiasi ni matajiri na bado wanataka kuwa matajiri inafikia wanauacha utajiri bila ya kuufaidi. Neema inatufundisha tuenende kwa kiasi hata katika tabia zetu za kawaida, Mungu anataka tuwe watu wa utaratibu," amebainisha.