Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waandishi wa habari watakiwa kutangaza vivutio Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa huo (hawako pichani ) katika maadhimisho ya siku ya waandishi wa habari yaliyofanyika Mkoani humo. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (RC), Stephen Kagaigai amelitaka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa) kuwatumia waandishi wa habari wa mkoa huo kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo.

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (RC), Stephen Kagaigai amelitaka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa) kuwatumia waandishi wa habari wa mkoa huo kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo.

Kaigaigai ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 16, 2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyoadhimishwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro (MECKI).

Amesema Mkoa huo una vivutio vingi ikiwamo Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Mkomazi, Mlima Shengena, Ziwa Challa na Mapango yaliyopo chuo cha Wanyamapori Mweka hivyo ametaka vitangazwe ili viweze kufahamika kimataifa na kukuza utalii nchini.

"Kama mnavyojua, Rais wetu alishiriki katika utengenezaji wa filamu ya Royal Tour ambayo aliizindua hivi karibuni nchini Marekani na hapa nchini, kupitia filamu hii ninyi waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro mnayodhamana kubwa kuhakikisha mnavitangaza kwa kina vivutio vyetu vilivyopo hapa kwetu Kilimanjaro ili kuvutia zaidi watalii kutoka Mataifa mbalimbali,"

"Ni vyema wanahabari kujikita katika kuandaa habari na makala mbalimbali zenye kuelezea vivutio vilivyopo mkoani hapa ambavyo vitalisaidia Taifa katika kuingiza fedha za kigeni naamini mna nafasi kubwa sana katika kutekeleza hili"amesema Kagaigai

"Katika kutekeleza hili napenda kulielekeza Shirika la Hifadhi za Taifa hapa nchini (Tanapa) na (Kinapa) kupitia hifadhi zake zote zilizopo kanda ya Kaskazini hususani za Mkoa wa Kilimanjaro kushirikiana na waandishi wa habari kutangaza vivutio vilivyopo katika mkoa huu,"amesema Kagaigai

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani humo, Bahati Nyakiraria amesema chama hicho kitaendelea kushirikiana na Serikali ya mkoa huo katika kuchangia maendeleo ya mkoa kwa kutumia taaluma zao.

"Serikali ya Mkoa wetu wa Kilimanjaro imekuwa ikitutendea haki katika kulisukuma gurudumu la habari na kusonga mbele na tutaendelea kutumia taaluma zetu za uandishi wa habari katika kuleta maendeleo ya mkoa wetu," amesema Nyakiraria