Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waandishi wa habari watakiwa wasome vifungu vya sheria yao

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mwezeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mpya za vyombo vya habari yaliyoandaliwa na Misa-Tan

Muktasari:

Wadau wa habari nchini wamewataka waandishi wa habari kutotumia vibaya uhuru uliopo kwa sasa kwani sheria zilizokuwa zikitumika katika awamu zilizopita ziko palepale.

Arusha. Wadau wa habari nchini wamewataka waandishi wa habari kutotumia vibaya uhuru uliopo kwa sasa kwani sheria zilizokuwa zikitumika katika awamu zilizopita ziko pale pale na badala yake wasome sheria hizo ili yapatikane maoni sahihi pindi maboresho yatakapofanyika.

Hayo yamesemwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu  sheria mpya za vyombo vya habari ikiwemo Sheria za Huduma za Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016 yaliyoandaliwa na Misa-Tani  na kufanyika  mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Jesse Kwayu amesema sheria za vyombo vya habari zikifanyiwa maboresho zitawapa nafasi waandishi wa habari kufanya kazi zao bila uoga.

"Sheria zipo pale pale kilichobadilika tu ni utawala na utawala huu unaonekana kuvumilia na kukubali watu kuzungumza na kuzungumza ni miongoni mwa haki za binadamu. Awamu hii inaheshimu na kutambua uhuru lakini haimaanishi kwamba tuko salama kwa sababu zile sheria kandamizi ambazo tuliona zikitumika vibaya bado zipo,"

"Ni vizuri sheria hizi zikafanyiwa mabadiliko ili kujenga mazingira bora kwa ajili ya ustawi mzuri kwa vyombo vya habari ili waandishi wa habari waweze kufanya kazi zao bila kuogopa kama ilivyokuwa hapo awali," amesema Kwayu.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Misa-Tan, Mussa Juma amesema ni vyema kila mwandishi wa habari akasoma vifungu vya sheria vilivyopo ili waweze kujua mapungufu yaliyopo ili yaweze kuingizwa kwenye mchakato wa maboresho ya sheria.

"Katika chambuzi mbalimbali zilizofanywa vipo vifungu kama 16 vya sheria ya vyombo vya habari ambavyo vinatakiwa vifanyiwe maboresho. Hivyo tunaomba waandishi wa habari wavisome, wavielewe ili serikali inapotaka maoni yapatikane maoni sahihi kutoka kwa waandishi wa habari," amesema Mussa.