Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wabainisha ‘mzigo’ wa rais mpya TLS

Wabainisha ‘mzigo’ wa rais mpya TLS

Muktasari:

  • Uchaguzi Mkuu wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) unatarajiwa kufanyika Aprili 15 jijini Arusha, ambapo miongoni mwa changamoto kubwa ambazo zinatakiwa kutatuliwa na uongozi ujao ni kurejesha uhuru, umoja miongoni mwa mwao na kuboresha sheria na kanuni.

Arusha. Uchaguzi Mkuu wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) unatarajiwa kufanyika Aprili 15 jijini Arusha, ambapo miongoni mwa changamoto kubwa ambazo zinatakiwa kutatuliwa na uongozi ujao ni kurejesha uhuru, umoja miongoni mwa mwao na kuboresha sheria na kanuni.

Wakizungumza na Mwananchi, mawakili waandamizi, Alute Munghwai na Dk Elifuraha Laltaika, walisema Rais ajaye wa TLS na baraza la uongozi wanapaswa kurejesha umoja wa wanasheria na kuwa na uwezo kuwatetea wenzao, hasa kutokana na maboresho ya kanuni na sheria ambazo tayari zimepitishwa na Bunge.

Munghwai alisema kutokana na mabadiliko ya sheria ya TLS yaliyofanywa na Bunge hivi karibuni bila ridhaa ya wanachama, mkutano wa mkuu kuanzia mwakani utashirikisha wajumbe wachache ambao watatokana na viongozi wa mikoa na kanda badala ya wanachama wote.

“Mabadiliko haya si tu yataondoa sauti ya pamoja ya mawakili lakini pia, hayatokani na mawazo ya mawakili wengi ambao walikuwa wakipenda wote kukutana katika mikutano mikuu kujadili mambo yao na kuwa na sauti ya pamoja,” alisema.

Alisema mikutano iliyopita mawakili zaidi ya 1,500 walikuwa wanashiriki, lakini sasa kwa mabadiliko haya mikutano mikuu itahudhuriwa na wajumbe chini ya 200 ambao ni rahisi kuwadhibiti.

Alisema changamoto nyingine ni kamati za maadili, ambapo sasa masuala ya kimaadili ya mawakili yatasikilizwa na kamati mikoani ambapo wajumbe wengi watatoka katika vyombo vya Serikali huku mawakili binafsi wakiwa na mjumbe mmoja.

“Hili jambo bado ni changamoto kwa uongozi ujao, ni muhimu kurejesha uhuru wa mawakili kwani sasa kuna chombo kinaweza kuwachukulia hatua, ambacho hakina uwakilishi mzuri wa mawakili binafsi. Kazi kubwa viongozi wajao wanaweza kwenda Mahakama Kuu kupinga baadhi ya marekebisho haya,” alisema.

Kwa upande wake, Dk Laltaika ambaye ni mhadhiri Chuo kikuu cha Makumila, alisema uongozi mpya una changamoto ya kuhakikisha mabadiliko ya sheria na kanuni mbalimbali hayaendi kuondoa uhuru, umoja na mshikamano wa mawakili.