Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadaiwa kuingilia mifumo ya benki, kujipatia Sh1.6 bilioni

Muktasari:

  • Washtakiwa hao wanadaiwa kuiba fedha hizo katika miji ya Arusha, Dar es Salaam na nchi za Ghana, Uganda na Ivory Coast, baada ya kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya BancABC.

Dar es Salaam. Raia wa Ghana, Valentine Zancheus (42) na Mtanzania, Fortunatus Bundala (36) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuingilia mifumo ya benki ya BancABC na kujipatia na Sh1.6 bilioni mali ya benki hiyo.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao, leo Julai 31, 2023 na wakili wa Serikali Clemence Mango, mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi.

Wakili Mango, amedai katika shtaka la kwanza ambalo ni kula njama ya kutenda kosa la wizi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba Mosi, 2021 na Julia 31, 2022 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nje ya nchi.

Shtaka la pili ni kuingilia mifumo ya kompyuta ya benki hiyo, tukio wanalodaiwa kulifanya ndani na nje ya nchini.

Inadaiwa siku hiyo, katika maeneo ya ndani ya Tanzania na nje ya nchini, washtakiwa bila halali walioingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya African Banking Corporation Tanzania Limited (BancABC).

Pia katika tarehe hizo, katika miji ya Arusha, Dar es Salaam na nchi ya Ghana, Uganda na Ivory Coast, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuiba Sh1.6 bilioni kutoka katika benki ya BancABC, kwa kutumia Visa.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakili hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalum.

Upande wa mashtaka wamedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanaomba terehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali (PH).

Hata hivyo washtakiwa hao waliomba Mahakama hiyo iwape dhamana.

Hakimu Kyaruzi alitoa masharti ya dhamana ambayo kila mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwenye Taasisi inayotambuliwa kisheria watakaowasilisha fedha taslimu Sh400 milioni au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia washtakiwa hao hawatakiwi kutoka nje ya nchini bila kibali cha mahakama na hati zao za kusafiria ziwasilishwe mahakamani hapo.

Hata hivyo, washtakiwa hao, wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 14, 2023.