Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadaiwa sugu MRT-Saccos waonywa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro, Jacqueline Senzighe ametoa karipio kali kwa baadhi ya wanachama wa Saccos ya walimu Moshi Vijijini (MRT-Saccos) ambao wanadaiwa madeni sugu zaidi ya Sh107 milioni huku akisema majina yao yatabandikwa kwenye shule wanazofundisha.

Moshi. Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro, Jacqueline Senzighe ametoa karipio kali kwa baadhi ya wanachama wa Saccos ya walimu Moshi Vijijini (MRT-Saccos) ambao wanadaiwa madeni sugu zaidi ya Sh107 milioni huku akisema majina yao yatabandikwa kwenye shule wanazofundisha.

Ameyasema hayo leo Desemba 13, 2021 wakati wa mkutano mkuu wa 24 wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Walimu Moshi vijijini (MRT-Saccos) uliofanyika katika ukumbi wa YMCA uliopo Manispaa ya Moshi.

"Nawasihi wale wanachama ambao hawatumii huduma za kwenye chama ni wakati sasa wa kutumia huduma za chama, hakikisha fursa inavyotoka chamani changamkia na itumie ili mwisho wa siku uwe mmojawapo wa kuchangia faida za chama lakini na mwisho wa siku utapata gawio la mwisho wa mwaka,” amesema na kuongeza

"Napongeza kamati ya usimamizi wamekuwa wakweli katika taarifa yao hasa kwenye suala la mikopo, kwenye mapendekezo wameshauri kamati ya mikopo kufuatilia wadaiwa sugu, sasa tutashangaa ndani ya saccos ya wafanyakazi tunawadaiwa sugu yaani saccos za jamii zitupe shida alafu saccos ya wafanyakazi itupe shida"

"Huku ni kujishushia hadhi, natoa rai tuendelee kuwa kioo kizuri kwa jamii wale ambao mnaturudisha nyuma majina yatabandikwa shuleni na ofisi kuu na tutadili nao vizuri" amesema Senzighe

Ameipongeza bodi ya chama hicho cha walimu na menejimenti kwa ujumla katika kufanikisha hesabu za chama hicho na kuwa miongoni mwa Saccos zinazofanya vizuri nchini.

Naye Mwenyekiti wa bodi wa chama hicho, Simon Minga amesema licha ya mafanikio makubwa waliyonayo kumekuwepo na mabadiliko ya mfumo wa makato ya mikopo kwa mwajiri (Epicor 10) ambayo yamepelekea kuwepo na makosa mengi kwenye makato ya mikopo ya wanachama.

"Uongozi wa bodi unawapongeza wanachama wote wanaorejesha mikopo kwa wakati ili kuwawezesha huduma kwa wanachama wengine, chama kimejizatiti kuwafuatilia wadaiwa wa mikopo yote chechefu," amesema Minga