Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadakwa wakidaiwa kutorosha dhahabu kilo 7.9

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumamosi Oktoba 28, 2023. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kikosi kazi cha Tume ya Madini, linawashikilia watu watano wakidaiwa kutorosha vipande 160 vya madini vyenye uzito wa gramu 6,933.6 sambamba na kufanya biashara hiyo bila kibali.

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kikosi kazi cha Tume ya Madini, linawashikilia watu watano wakidaiwa kutorosha vipande 160 vya madini vyenye uzito wa gramu 6,933.6 sambamba na kufanya biashara hiyo bila kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema leo Jumamosi Oktoba 28, 2023 na kuwataja watuhumiwa kuwa ni  Masunga Kidishi (43), Timoth Simbu (26), Ngunje Ideshi (41), Ester John (25), na Baraka Silwani ( 28) ambao wote ni wafanyabishara na wakazi wa Chokaa Wilaya ya Chunya.

Amesema watuhumiwa walikamatwa Oktoba 26, 2023 katika Mtaa wa Kibaoni, wilayani Chunya wakiwa na vipande hivyo vya madini ya dhahabu, ambapo walikuwa wanavitorosha ili wakaviuze nje ya mfumo wa soko la dhahabu.

“Nitoe onyo kwa wachimbaji, Jeshi la Polisi hatutawafumbia macho watu wanaojihusisha na utoroshaji wa madini, kwani kunachangia kupoteza mapato ya Serikali ambayo yanapaswa kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.

Kuzaga amesema kuwa watuhumiwa wamekiri kuhusika na utoroshwaji wa madini hayo na kwamba uchunguzi unaendelea watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Wakati huo huo, jeshi hilo linawashikilia wahamiaji haramu 11 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na kibali.

Watuhumiwa walikamatwa Oktoba 27, 2023 eneo la Igawa Wilaya ya Mbarali katika barabara Kuu ya Mbeya - Njombe wakati Askari wakiwa doria.

Watuhumiwa walikuwa wakisafirishwa kwa kutumia Toyota Mark X rangi nyeupe ambalo lilikuwa likiendeshwa na Frank Makunde (38), mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe ambaye pia amekamatwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wafanyabiashara wa madini kufuata utaratibu wa kuuza na kununua madini katika masoko yaliyopo kwa mujibu wa sheria ili kuepuka usumbufu.

Mkazi wa Jijini hapa, Ernest Joel amesema kuwa changamoto kuwa ya utoroshwaji wa madini ni kutokanana utitili wa tozo kwenye Soko la madini na ndio sababu ya wachimbaji kuingia katika mitukio ya kutorosha na kusababisha Serikali kukosa mapato.