Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau waikumbusha Serikali kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa

Muktasari:

  • Watetezi wa haki za watoto wameitaka Serikali kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa kwa ridhaa ya mzazi kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya msingi iliyofunguliwa na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Msichana Initiative, Rebeca Gyumi.

By Janeth Jovin

Dar es Salaam. Watetezi wa haki za watoto wameitaka Serikali kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa kwa ridhaa ya mzazi kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya msingi iliyofunguliwa na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Msichana Initiative, Rebeca Gyumi.

 Mwanzoni mwa mwaka 2016,  Rebeca kupitia kwa wakili Jebra Kambole walifungua kesi kupinga kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Julai 8, 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ikikubali kwamba vifungu hivyo vya sheria ya ndoa vinapingana na Katiba ya nchi kwa kuweka umri tofauti wa kuoa na kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2021, mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu wa  Taasisi ya Kujenga Jamii Jumuishi Tanzania (BISTO), Mussa Nzige amesema licha ya Serikali kupewa mwaka mmoja na mahakama kuibadilisha sheria hiyo mpaka sasa bado hajatekeleza amri hiyo.

Amesema kuelekea siku ya mtoto wa Afrika dunia inayoadhimishwa kila Juni 16 ya kila mwaka,  wanaitaka Serikali kufanya marekebisho hayo ya sheria kama ilivyoamuliwa na mahakama.

“Katika hukumu ya mahakama iliitaka Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele hivyo tata vya sheria ndani ya mwaka mmoja, muda umeshapita tangu amri hiyo itoke na hakuna jitihada zozote zilizofanyika katika kutekeleza maamuzi hayo.”

“Ndio maana sisi wadau kwa pamoja tumekutana na kuitaka Serikali kuifanyika marekebisho sheria hiyo ambayo ni ya kibaguzi  kwa watoto wa kike na wa kiume,” amesema Nzige.

Nzige amesema siku ya mtoto wa Afrika yenye kauli mbinu ya ‘Tutekeleze ajenda 2040 kwa Afrika imfaayo Mtoto’ huadhimishwa kila mwaka ili kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto katika jamii wanazoishi na kuweza kuwaondolea.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Kupinga Ukatili wa Kijinsia (CAGBV), Sophia Komba amesema katika utekelezaji wa ajenda ya 2040 kundi la watoto wenye ulemavu bado limekuwa na changamoto zinazowafanya wasifurahie utoto wao kama watoto wengine.

"Kundi hili la watoto wenye ulemavu limekuwa likisahaulika bila ya kutajwa kwa upekee wake kama kundi maalum. Kwa kutumia siku hii tungependa kutaarifu jamii kuhusu ulinzi na changamoto kwa watoto wenye ulemavu.”

“Nchini Tanzania inakadiriwa kuwa na watoto wenye ulemavu, walio shuleni na wasio shuleni. Serikali imeweza kutoa huduma mbalimbali kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuwalinda mfano kuandaa sera na kusaini mikataba kama vile haki kwa watu wenye Ulemavu (1975), Haki za Mtoto (1989) na Haki na Fursa sawa kwa Watu wenye Ulemavu (1993), uboreshaji wa miundombinu,” amesema