Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walichozungumza Rais wa Tanzania, Msumbiji

Muktasari:

  • Marais wa Serikali ya Tanzania, Msumbiji wameweka wazi makubaliano yao baada ya mazungumzo yao yaliyolenga kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili


Dar es Salaam. Marais wa Serikali ya Tanzania, Msumbiji wameweka wazi makubaliano yao baada ya mazungumzo yao yaliyolenga kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili

Marais hao leo Jumatano Septemba 21, 2022 wamezungumza na vyombo vya habari katika Ikulu ya Msumbiji jijini Maputo wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya Kiserikali ya siku tatu nchini humo na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Filipe Nyusi.

Akizungumza katika hotuba yake, Rais Samia amesema mahusiano ya eneo la biashara na uwekezaji yanahitajika kutokana na kushuka kwa biashara kutoka wastani wa Sh53 bilioni mpaka Sh36 bilioni mwaka huu.

“Hili ni eneo muhimu ambalo tunahitaji kulifanyia kazi na tumekubaliana namna ya kutumia fursa za biashara na uwekezaji kama kilimo, uvuvi na uchimbaji madini,” amesema.

Eneo la elimu, Rais Samia amesema kutakuwa na ushirikiano wa kubadilishana wanafunzi wa elimu ya juu kurahisisha ushirikiano wa vijana kuishi pamoja ili kukuza mawasiliano yetu.

“Tutaendelea na ufundishaji wa Kiswahili nchini Msumbiji ili tutumie lugha moja na watu wa Msumbiji kuzungumza vizuri Kiswahili. Naamini ziara yangu hii itafungua mashirikiano mapya baina ya Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji ili kuweza kuleta ustawi na kanda yetu kwa ujumla,” amesema RaIS Samia.

Rais Nyusi amesema watatumia ukaribu wa nchi hizo kushirikiana katika mazungumzo na eneo la nishati na mapambano dhidi ya ugaidi.

“Kufuatilia suala la demokrasia hasa katika kipindi hiki cha ugatuaji wa madaraka na mahusiano kati ya Serikali. Eneo la utalii itatusaidia mahusiano ya karibu kati ya nchi hizi mbili, yamejikita maeneo ya uchumi kuna namna ya kustawisha jamii yetu,” amesema Rais Nyusi.