Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliokatisha masomo 1,907 warejea shuleni

Muktasari:

  • Mbunge wa Viti Maalum Tunza Malapo amehoji idadi ya wanafunzi waliorejeshwa shuleni katika utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka wanafunzi waliokatisha masomo kurejeshwa.

Dodoma. Hadi Januari mwaka huu, jumla ya wanafunzi 1,907 waliokatiza masomo ya sekondari wamerejeshea shuleni tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipotoa uamuzi huo.

Juni 2017 Rais wa awamu ya tano John Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari.

Hata hivyo Novemba 24 mwaka 2021, Rais Samia Suluhu Hassan aliruhusu wanafunzi wanaokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito kurejea shuleni na kuendelea na masomo kwa mfumo rasmi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga wakati akijibu swali la msingi wa Mbunge wa Viti maalum Tunza Malapo.

Mbunge huyo amehoji ni wanafunzi wangapi wamerejea shuleni tangu waraka wa kuwaruhusu utolewe.

Akijibu swali hilo, Kipanga amesema mpaka kufikia Januari, 2023 wanafunzi waliorejea shuleni kuendelea na masomo ya elimu ya Sekondari ni 1,907.

Amesema kati ya hao waliorudi katika mfumo rasmi ni 562 na waliorejea nje ya mfumo rasmi wa elimu kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ni 1,345.

Amesema Serikali inaendelea kukusanya taarifa za wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu mbalimbali.

Katika swali la nyongeza, Tunza amehoji Serikali inampango gani wa kupunguza muda wa wahitimu wa kidato cha nne kusubiri kwenda kidato cha tano.

Akijibu swali hilo Kipanga amesema ni kweli kwa muda wa takribani miezi saba wanafunzi hao husubiri kwenda katika masomo ya kidato cha tano.

Amesema katika kipindi hicho wanakitumia kwenye usahishaji na uteuzi wa wanafunzi na upangaji wa wanafunzi kwenye shule za kidato cha nne.

Amesema hivi sasa wataanza usahishaji na upangaji wa wanafunzi kwa njia ya kieletroniki ili kupunguza muda wa shughuli hizo ili waweze kuufanyia kazi.