Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi wanusurika, moto ukichoma bweni

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Rajab Mkasaba amesema licha ya moto huo kutoleta hakuna vifo wala majeruhi, bali umeteketeza vifaa vya wanafunzi hao.

Unguja. Wanafunzi zaidi ya 200 wamenusurika kuungua baada ya bweni la shule ya sekondari ya Khasnuu Makame Mkoa wa Kusini Unguja kuteketea kwa moto.

 Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Oktoba 13, 2023 baada ya moto huo kuteketeza bweni hilo la wasichana wakati wakiendelea kujisomea madarasani.

Akizungumza na Mwananchi digital kwa njia ya simu leo Oktoba 13, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Rajab Mkasaba amesema licha ya moto huo kutoleta hakuna vifo wala majeruhi, bali umeteketeza vifaa vya wanafunzi hao.

“Ni kweli bweni hilo limeteketea kwa moto lakini tunashukuru MUngu hakuna madhara ya vifo wala kujeruhiwa kwa wanafunzi, wakati moto unatokea wanafunzi walikuwa wakiendelea na masomo darasani,” amesema Mkasaba

Amesema jeshi la zimamoto kwa kushirikiana na watu wengine wanaotoa huudma za maji walifika kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kudhibiti moto huo licha ya sehemu kubwa ilikuwa tayari imeshateketea

Bweni hilo lenye ghorofa mbili, limeungua sehemu ya juu kabla ya moto kudhibitiwa na kusambaa maeneo mengine.

Kwa mujibu wa Mkasaba wanafunzi zaidi ya 130 wamepewa mapumziko ya muda hadi Jumatatu Oktoba 16 ili kupumzisha akili wakati serikali ikifanya jitihada za kuhakikisha inarejesha mazingira ya bweni hilo katika mazingira ya kawaida kwa kushirikiana na wadau.

Huu ni mwendelezo wa matukio ya moto kutokea mfululizo katika wilaya na Mkoa huo.

Julai 9, 2023 hoteli tano ziliungua kwa moto kabla ya Agosti 4, hoteli eli nyingine ya Karibu Beach Resort Pongwe wilaya ya Kati ikiungua kwa moto.

Katika matukio hayo yote hakuna aliyejeuhiwa wala kupoteza maisha mbali na kuharibu tu mali.

Hoteli zilizoungua Julai 9, 2023 ni Cristal resort, Merak, Maisha Matam, Drifters na The Nest Boutique resort ulipoanzia moto huo na kusambazwa na upepo kwenye hoteli nyingine kutokana na kuezekwa kwa makuti.