Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi watembea kilometa 10 kufuata masomo

Mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga wapili kulia akiwa na viongozi wengine walipotembelea eneo lilitolewa na wananchi wa kata ya Ruhuhu kwaajili ya ujenzi wa shule ya sekondari.

Muktasari:

  • Wananchi wa Kata ya Ruhuhu wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe wameiomba Serikali kuwajengea shule ya sekondari.

Ludewa. Ikiwa mkakati moja wapo wa sekta ya elimu ni kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi kujisomea, watoto kutoka Kata ya Ruhuhu Wilayani Ludewa wanalazimika kusafiri umbali wa 10 km kufuata elimu ya sekondari.

Hayo yameelezwa na Lenard Komba mkazi wa Kijiji cha Kipingu, Kata ya Ruhuhu aliyetoa sehemu ya eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa shule.

“Nimetoa eneo langu kwa sababu watoto wanapata tabu kwenda shule Manda na kurudi sababu wanatembea Kilomita 10 kwenda shule tu wakati shule ingejengwa kwetu wasingeteseka,” amesema Komba.
Ameongeza kuwa wao kama wananchi wapo tayali kushiriki shughuli zote za ujenzi ili kuwa nusuru wanafunzi hao.
“Tumekubali kujitolea kushiriki kazi zote za ujenzi wa hii shule, tumeshatoa eneo na tumeshaanza kuandaa tofali, tunaomba serikali ituunge mkono tufanikishe ndoto yetu,” amesema Komba.
Afisa Elimu Kata ya Ruhuhu, Upendo Chilambo amebainisha kuwa kwa mwaka Kata ya Ruhuhu hufaurisha wanafunzi wasiopungua 100 na hupelekwa Shule ya Sekondari Manda.
“Kata ya Ruhuhu ina shule za msingi tatu wanaofanya mitihani ya kumaliza darasa la saba sio chini ya 100, kwa mfano mwaka jana walifanya mitihani wanafunzi 111 na kuchaguliwa kwenda sekondari ambao wangetosha kwenye madarasa yetu hapahapa kama tungekuwa na shule ya sekondari,” Amesema Chilambo.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruhuhu, Yusuph Lukuwi amesema kiu kubwa ya wananchi hao ni shule ya sekondari ndiyo mana wameshaanza kujitolea nguvu zao.
“Kiu kubwa ya wana Ruhuhu ni shule ya sekondari ndio mana wametoa maeneo yao ekari 15 kwa ajili ya ujenzi wa shule. Wameshafyatua tofali laki mbili na elfu kumi, na fedha taslimu iliyoandaliwa ni milioni mbili na wapo tayali kujitolea nguvu zao ili shule ipatikane,” amesema Lukuwi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Wise Mgina amewaahidi wananchi kuwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani itatenga fedha za kukamilisha madarasa mawili na iwapo watafanya vizuri wataongezewa madarasa mengine hadi shule itakapokamilika.

Naye Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga amewaahidi wananchi hao kushirikiana nao mpaka shule itakapojengwa na kuanza kupokea wanafunzi kutoka kata hiyo na maeneo mengine.