Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi wawili wafariki kwa kutumbukia kwenye tenki la maharage

Muktasari:

  • Wanafunzi hao wanadaiwa kufariki baada ya kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye pipa kutoa maharage.

Moshi. Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia baada ya kudaiwa kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye tenki la kuhifadhia maharage.

 Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kileuwo wilayani hapa, Godfrey Mrema amesema tukio hilo limetokea Mei 12, 2023, wakati wanafunzi hao walipoingia kwenye tenki hilo kwa ajili ya kutoa maharage ya chakula shuleni.

“Wanafunzi hao wote wana umri wa miaka 17, na uongozi wa shule umesema wote walifariki baada ya kuingia kwenye tenki kwa ajili ya kutoa maharage ya kupeleka stoo kwa ajili ya kupika,” amesema.

Ameongeza kuwa “Kwa taarifa tuliyoipata shuleni ni kwamba wanafunzi hao walipanda kwenye pipa hilo kwa kutumia ngazi na kisha kutumbukia ndani kutoa maharage na alianza kuingia mmoja, halafu akaanza kupiga kelele ndipo mwenzake akaingia kwa ajili ya kumuokoa lakini walikosa hewa na hadi kugeuza pipa kutolewa walishafariki,” amesema.

“Hapa inaonekana kuna uzembe, maana kama shule ina mpishi, kwa nini wanafunzi waingie kwenye pipa kwa ajili ya kutoa maharage kupeleka stoo? Alihoji mwenyekiti huyo na kueleza kuwa, tayari vyombo vya usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya walifika eneo la tukio.

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori kuzungumzia tukio hilo, amesema atalizungumzia baadaye.