Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi 40,000 kunufaika na mradi wa maji Mtama

Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi huo wa maji mkoani Lindi. Picha na Bahati Mwatesa.

Muktasari:

Mradi unatekelezwa kwa miaka sita na kwa awamu tofauti, awamu ya kwanza utatekelezwa kwa miaka mitatu katika Halmashauri ya Mtama na malengo ni kufikia vijiji 87 na kaya zaidi ya 40,000.

Lindi. Zaidi ya wakazi 40,000 wa Halmashauri ya Mtama watanufaika na mradi wa maji na usafi wa mazingira wenye thamani ya Sh1 bilioni unaotekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya “Heart to Heart” iliyo chini ya mwavuli wa Shirika la Kimataifa la KOICA.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo leo Mei 20, 2024, mratibu wa mradi, Innocent Deus amesema mradi unatekelezwa kwa miaka sita na kwa awamu tofauti, awamu ya kwanza utatekelezwa kwa miaka mitatu katika Halmashauri ya Mtama na malengo ni kufikia vijiji 87 na kaya zaidi ya 40,000.

Deus amewataka viongozi wanaohusika na usimamizi wa mradi kuhakikisha usafi unazingatiwa kuanzia ngazi ya vijiji hadi halmashauri ili malengo ya kupeleka mradi katika halmashauri ya Mtama na kupeleka huduma ya maji kwenye vituo vya afya unatimia.

“Mradi huu utanufaisha wananchi zaidi ya 40,000 wa halmashauri ya Mtama, niwatake wananchi mradi unapoanza wajitahidi kuutunza ili uweze kuwasaidia kwa muda mrefu na pia tutahakikisha vituo vyote vya afya vilivyopo halmashauri ya Mtama vitakuwa na maji ya uhakika,” amesema Deus.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Zuwena Omary amewataka wananchi wa halmashauri ya Mtama wakishirikiana na taasisi mbalimbali zilipo kwenye halmshauri hiyo, kuhakikisha wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.

“Niwaombe watu wa Mtama kujitahidi kutunza vyanzo vya maji, hii itatusaidia wenyewe, mjitahidi kupanda miti kuzunguka vyanzo vya maji ikiwemo upandaji miti na nizitake kamati zote za maji zishirikishwe ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,” amesema Omary.

Ismail Bani, Ofisa Afya na Mazingira katika halmshauri ya Mtama,  amesema unawaji wa mikono katika halmashauri ya Matama ni asilimia saba tu licha ya Serikali kujitahidi kuweka miradi mingi ya maji. Amesema mwitikio ni mdogo katika njia hiyo ya kujikinga na maambukizi.

Anna Emily, mkazi wa halmashauri ya Mtama amesema wananchi waanze kupewa elimu kabla ya mradi utakapoanza hiyo itasaidia kuweza kuuthamini mradi kwa kutunza vyanzo vya maji na kuweza kukaa kwa muda mrefu.

“Elimu inatakiwa kutolewa kwa wananchi kwani sio wote tutakuwa na uelewa sawa, kila mtu ana akili yake, wakiweza kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi nina imani mradi utadumu sana na hakuna atakayeweza kuuharibu,” amesema Anna.