Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi Igoma wachanga Sh60 milioni kujenga kituo cha polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna msaidizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga akizungumza wananchi wa  Kata ya Igoma  Wilaya ya Mbeya nje ya kituo cha Polisi kilichojengwa kwa nguvu zao.Picha na Hawa Mathias

Muktasari:


  • Wananchi wa Igoma, Mbeya, wachangia Sh60 milioni kujenga kituo cha polisi kutokana na umbali wa kilometa 25 hadi kilipo kituo cha polisi.

Mbeya. Wananchi wa kijiji cha Igoma kilichopo Kata ya Igoma mkoani Mbeya, wamelazimika kuchanga Sh60 milioni na kutumia nguvu kazi zao kujenga kituo cha polisi kuepuka adha ya kutembea umbali wa kilometa 25 kufuata huduma hiyo katika kata ya Inyala.

Kata hiyo ina vijiji vitatu---Igoma, Kimoto na Mwanzazi huku kukiwa na wakazi 6,172 kutoka kaya 1,736 ambao kwa kipindi kirefu wamekosa kituo cha polisi.

Diwani wa Igoma, Caritas Mwaipopo amemueleza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga alipotembea ujenzi wa kituo hicho leo Jumapilil Machi 10, 2024 na kuzungumza na wananchi hao.

“Niwashukuru wananchi kwa hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi, hali ambayo itapunguza adha ya kutembea umbali mrefu,” amesema.

Amesema ujenzi umefika hatua hiyo ni kutokana na michango ya wananchi, hususan kutumia nguvu kazi huku zaidi ya Sh100 milioni zikihitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo, ili kianze kufanya kazi.

Muonekano wa kituo cha polisi kilichojengwa kwa nguvu za wananchi Kata ya Igoma Wilaya ya Mbeya

Kwa upande wake, Kamanda Kuzaga amewapongeza wananchi wa kata ya Igoma iliyopo wilaya ya kipolisi Mbalizi mkoani Mbeya kwa kushiriki katika ujenzi wa kituo cha polisi.

Pia ameushukuru uongozi wa kata ya Igoma kwa kutoa eneo na kuanza ujenzi wa kituo cha polisi ambao umefikia hatua ya mwisho.

Wakati huohuo, amewataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika suala la malezi bora kwa watoto, ili kuwafanya wakue katika misingi mizuri ya ustawi wa jamii na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.