Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi KIA ‘wamlilia’ Rais Samia kuingilia kati mgogoro wa eneo

Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe akizungumza na wananchi wa kata ya Kia kujadili namna ya kumaliza mgogoro wa mpaka uliopo baina yao na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA). Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Wananchi wa vijiji vitano vinavyouzunguka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) wameiomba Serikali kutowaondoa kwenye eneo hilo kwa kuwa ni wazawa wa eneo hilo.

Hai. Wananchi wa vijiji vitano vinavyouzunguka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) wameiomba Serikali kutowaondoa kwenye eneo hilo kwa kuwa ni wazawa wa eneo hilo.

Eneo hilo lenye ukubwa wa hekari zaidi ya 11,000 lina mgogoro kati ya wananchi na uwanja huo wa ndege ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 20 na bado halijapatiwa ufumbuzi licha baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali kufika katika eneo hilo kwa wakati tofauti.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kia, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wamemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kusema wako tayari kukaa meza moja na kiongozi yoyote kujadili mwafaka wa mgogoro huo na kupata ufumbuzi.

Akizungumza katika mkutano huo, Laitness Laizer ambaye ni mkazi wa kata ya KIA, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro huo na kuuona namna ya kuumaliza kwa kuwa wapo kwenye eneo hilo kwa miaka mingi.

"Rais Samia Suluhu Hassan huko ulipo sisi ni wananchi wako, tunakuona unavyopambana kwa ajili ya wananchi wako wa Tanzania, tunaomba hili suala la mgogoro ambao umekuwa ni wa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi uingilie kati mama yetu," amesema

"Tuangalie kwa jicho la huruma, wananchi wanaouzunguka uwanja wa KIA ni wengi na wanaumia, zipo kaya takribani 5000  tunaomba hili jambo ulitizame kwa jicho la pili hata kama hili eneo wanasema ni la uwanja wa ndege hebu fikiria jinsi litakapoweza kupunguzwa hataka kama hili eneo litahitajika na serikali, hatuna pakwenda na hata hatujui tutaanzia wapi," amesema

Samweli Mamasita amesema wapo tayari kukaa na wizara zote ili upatikane mwafaka wa kudumu kwa kuwa eneo hilo walishafika mawaziri mbalimbali na hawakuwahi kuwapa suluhisho ili wajue wako upande upi katika eneo hilo.

"Hatupingani na Serikali katika eneo hili lakini tunataka kujua mwafaka wa hili eneo kwa sababu tangu enzi na enzi sisi tumezaliwa na kukulia hapa, tunaomba tathmini ya hii mipaka ifanyike upya na sisi tuko tayari kuonyesha ushirikiano kwa kiongozi yeyote,"

Kwa upande wake, Mbunge wa Hai (CCM), Saashisha Mafuwe aliwataka wananchi hao kujipanga kwa lolote kwa kuwa Serikali inalihitaji eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya uwanja ikiwa ni pamoja na kujenga hoteli za kitalii pamoja na mambo mengine.

"Ndugu zangu mlinituma nikaongee na viongozi wa Serikali kuhusu mgogoro huu, na leo hii nimerudi mbele yenu kuwapa majibu, katika hili, msimamo wa Serikali ni kwamba inahitaji eneo lote lenye zaidi ya hekta 11,000 kwa ajili ya matumizi ya uwanja wa ndege.

“Tutaendelea kuongea na Serikali kama kweli uwanja huu bado mahitaji ni yale yale au haja ni kuhamisha vijiji vyote, niwaombe wananchi turuhusu wenzetu wa serikali wapite kwenye maeneo yetu wafanye tathmini," amesema mbunge huyo