Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wanufaika miradi ya elimu, afya mgodini

Muktasari:

  • Wananchi katika kata tano za Bugarama, Bukirilo, Kibogora, Muganza na Rulenge Wilaya ya Ngara wanufaika na mgodi wa uchimbaji wa Nickel wa Tembo Nickel kwa kujengewa miradi ya maendeleo ya afya na elimu yenye thamani ya Sh208 milioni.

Ngara. Meneja wa Kampuni ya Tembo Nickel inayohusika na uchimbaji madini ya Nickel Wilaya ya Ngara mkoani Kagera ameahidi kusaini mkataba ili kutekeleza miradi ya kijamii kwa mwaka 2023 huku akikabidhi miradi 11 iliyotekelezwa kwenye jamii mwaka 2022 yenye thamani ya zaidi Sh208.11 milioni.

 Miradi hiyo ya afya na elimu ya  uwabikaji kwa jamii imekabidhiwa leo Aprili  19, 2023 na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tembo Nickel, Manny Ramosh kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanali Mathias Kahabi.

Monash amesema richa ya kwamba kampuni hiyo bado haijaanza kuzalisha madini lakini mwezi Julai mwaka jana walisaini mkataba wa kutekeleza miradi ya uwabikaji kwa jamii (CSR) kati ya Kampuni ya Tembo Nickel na Serikali na miradi hiyo imekamilika kwa 100 asilimia.

"Mwaka jana Kampuni ya Tembo, Nickel tulisaini mkataba na serikali wa kutekeleza miradi ya uwabikaji kwa jamii na miradi hiyo imekamilika kwa 100 asilimia na mbali na kukabidhi miradi ya mwaka jana hata mwaka huu tunatarajia kusaini mkataba mwingine wa kutekeleza miradi ya kijamii," amesema Monash.

Kiongozi Idara ya Mahusiano Tembo Nickel,  Chiza Patrick ameitaja miradi iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa chumba cha darasa na madawati 20 Shule ya Msingi Mukivumu, ukarabati wa vyumba vinne vya madarasa Shule ya Msingi Ruhuba, vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu na madawati 20 Shule ya Msingi Gwenzaza, vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu na madawati 20 Shule ya Msingi Muganza.

Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa chumba  Cha darasa, ofisi ya walimu na madawati 20 katika shule ya msingi Nyabihanga, viti 80 na meza 80 Shule ya Sekondari Rulenge, kukamilisha ujenzi wa wodi ya wazazi na vifaa tiba zahanati ya Bugarama, kuweka vifaatiba Zahanati ya Rwinyana na mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika vijiji tisa.

Mmoja wa wananchi katika Kata ya Bugarama, Jasintha Buchwa amesema ujenzi wa wodi ya wazazi na kuwepo vifaa tiba katika Zahanati ya Bugarama itasaidia kina mama waliokuwa wanajifungulia nyumbani kutokana na jengo dogo kwenda kujifungulia zahanati kutokana na ujenzi wa jengo la wazazi na kuweka vifaa tiba.

Nikodemus Nicholaus mwalimu mkuu katika Shule ya Msingi Nyabihanga amesema, shule yake ina wanafunzi 585 alipata msaada wa kujengewa chumba cha darasa na ofisi ya walimu ambavyo vilighalimu Sh22 milioni na kuwa ujenzi huo umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi, shule yake ilikuwa na uhitaji wa vyumba vya darasa 15 na alikuwa navyo nane.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanali Mathias Kahabi amewaangiza viongozi wa vijijini na kata kusimamia miradi hiyo na kuwataka Tembo Nickel pale watakapokuta uharibifu kutoa taarifa kwake ili wale watakaohusika kuharibu miradi hiyo waweze kuwajibishwa.

Ikumbukwe kuwa mradi wa uchimbaji madini ya Nickel ulisainiwa mkataba na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Magufuli  Januari mwaka 2021 huku Tembo Nickel ikipaswa kufanya shughuli za uchimbaji madini kwa miaka 33.