Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanandoa Dar wahukumiwa miaka 30 jela

Mshtakiwa, Mwichande Said akitoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuhukumiwa kwenda miaka 30 jela jijini Dar es Salaam. Picha na Pamela Chilongola

Muktasari:

  • Mwichande Said (50) na Halima Maneno (39) wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela Kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 11.21.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mkazi wa Magomeni Mwichande Said (50) pamoja na mkewe Halima Maneno (39) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa gramu 11.21

Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo akitoa hukumu hiyo leo Julai 12, 2024 amesema baada ya Mahakama hiyo kupitia ushahidi wa mashahidi nane na vielelezo kumi wa upande Jamuhuri na utetezi wa washtakiwa hao imeridhika pasipo shaka lolote kutoka huku hiyo.

"Mahakama hii inawahukumu kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wenye vitendo kama hivyo," amesema Swalo.

Awali Wakili wa Serikali, Asiath Mzamiru aliieleza Mahakama hiyo kuwa adhabu kali itolewe kwa washtakiwa hao kulingana na sheria inavyotaka ili iwe fundisho kwa wale wenye tabia kama hiyo.

Baada ya Wakili Mzamiru kudai hayo, Hakimu Swalo aliwapa nafasi washtakiwa ili na wao waweze kuzungumza kuhusiana na suala la kupunguziwa adhabu walidai kuwa wanategemewa na familia pia wote wanaumwa ugonjwa wa kisukari hivyo Mahakama iwapunguzie adhabu.

Inadaiwa kuwa kati ya Machi 31, 2023 maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa wanasafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa gramu 11.21