Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaotumia VPN bila kibali faini Sh5 milioni, kifungo mwaka mmoja

Muktasari:

  • TCRA imeeleza kuwa kosa kwa anayetumia VPN bila kibali faini yake ni Sh5 milioni au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku matumizi ya mtandao binafsi (VPN) kwa wasiokuwa na kibali na anayegundulika atakumbana na adhabu ya faini au kifungo jela.

Taarifa ya katazo hilo imetolewa jana Oktoba 13,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari.

Taarifa hiyo ilisomeka "Kwa kuzingatia  kanuni ya 16(2) ya kanuni ya mwasiliano ya kielektroniki na Posta kuhusu maudhui  mtandaoni ya mwaka 2020, mtu hatatoa  hatamiliki na hatasambaza  teknolojia, programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na  ambacho kinaruhusu  au kumsaidia  mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa.

"Kwa kuwa TCRA imebaini upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kwa kupitia matumizi ya mtandao binafsi (VPN) kinyume cha kanuni.

"Hivyo tunautaarifu umma kuwa kampuni ambayo kwa asili ya majukumu na kazi zao, matumizi ya VPN hayazuiliki, kutoa taarifa kwa TCRA juu ya VPN wanazotumia na taarifa zote muhimu ikiwemo anuani ya itifaki ya mtandao (IP Adress) kabla ya ya Oktoba 30,2023," imeeleza  taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa TCRA itaendelea kuchukua hatua kudhibiti matumizi ya VPN yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa ambazo haijatolewa taarifa au kusajiliwa.

"TCRA inaukumbusha umma kuwa utoaji, umiliki au usambazaji wa teknolojia, programu, programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na ambacho kinaruhusu au kusaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa ni kosa la jinai.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kosa kwa anayekutwa na hatia ya matumizi ya VPN ni Sh5 milioni au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.