Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanasheria 50 watua Songwe kutatua changamoto za walionyimwa haki

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi akisikiliza maelekezo kutoka Banda la dawati la jinsia mkoa wa Songwe katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Picha na Denis Sinkonde

Muktasari:

  • Kampeni hiyo inatarajia kufanyika kwa siku tisa ambapo wananchi katika maeneo yao wataendelea kupata huduma za msaada wa kisheria.

Songwe. Jumla ya wataalamu wa kisheria 50 watua mkoani Songwe kwa lengo la kutoa huduma ya msaada wa kisheria itakayoanza kesho Desemba 12, 2024.

Wataalamu hao ni wale walio kwenye kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campain-MSLAC).

Akizungumza leo Desemba 11, 2024 na waandishi wa habari mjini Songwe kwa niaba ya Mkuu wa Mko wa Songwe, Daniel Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi,  kampeni hiyo itafanyika kwa siku tisa katika halmashauri zote tano za mkoa huo.

"Napenda kuwasihi wananchi wa Mkoa wa Songwe kujiandaa na baadaye kujitokeza kwa wingi wakati wa kampeni hii inayotarajia kufanyika kwa siku tisa,” amesema Mgomi.

Pia amewahimiza wote wenye changamoto za kisheria kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kufika na kuonana na wataalamu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

Akizungumzia lengo la kampeni hiyo, Mgomi amesema inalenga kutoa huduma za kisheria bure, huku akiyataja maeneo watakayozangatia ni pamoja na msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo vya unyanyasaji, kutetea mageuzi ya kisera ili kukuza usawa wa kijinsia na haki za kijamii.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Richard Kilanga amesema Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inalenga kutoa fursa kwa wale wote ambao wamenyimwa haki zao.

“Tunataka watu wawe na uwezo wa kudhibiti maisha yao, wasiache haki zao zikipotea, kwa kufanya hivi tutakuwa tumewajengea uwezo,” amesema Kilanga.