Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanasiasa wanawake kujadiliana sheria zitakazo wabeba

Muktasari:

  • Wanawake  kutoka vyama vya siasa nchini wakutana kujadili sheria zitakazowabeba kuwania nafasi mbalimbali ngazi ya maamuzi.

Dar es Salaam. Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed, amesema licha ya Kikosi Kazi kufanya kazi kubwa ya kuwasikiliza wadau walioibua hoja mbalimbali, lakini bado wanaendelea na mikutano mingine katika kuendea kuchaka hoja zingine.

Akizungumza Dar es Salaam kwenye mkutano ulioandaliwa Taasisi ya EFS uliowakutani wanawake kutoka umoja wa vyama vya siasa nchini waliokuwa unalenga kutoa elimu ya msukumo kwa wadau katika mchakato wa marekebisho ya sheria zote ambazo ziliguswa katika kikosi kazi zitekezwe.

 “Tulikuwa kwenye kikao cha pamoja cha muendelezo wa kuchakata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali katika suala nzima la ushirikishwaji  kwa wanawake katika vyombo vya maamuzi.
Kabla ya matukio haya kulikuwa na Kikosi Kazi ambacho kiliibua mambo mbalimbali kutoka kwa taasisi za umma na vyama vya siasa,”amesema

Amesema moja ya mambo yaliyoibuliwa katika kikosi kazi kile ni marekebisho ya sheria za uchaguzi, gharama za uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa ilionekana kuna ushiriki mdogo wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT)  akiwakilisha mkoa wa Dare es Salaam, Doreen Kahwa, alisema katika semina hiyo walikuwa wanapata elimu ya kuhusiana na kuongezeka fursa kwa kina mama katika vyama na uongozi.

“CCM tumepiga hatua ukiangalia nafasi nyingi za maamuzi zinashikwa na wanawake tangu na fasi ya Rais na Spika wa Bunge na  serikali imekuwa akitoa kipaumbele katika teuzi zake kuzingatia akina mama,”amesema

amesema kwa msingi huo serikali bado inaimani kubwa na mchango wa kina mama katika kufikia mageuzi ya kimaendeleo na kwamba elimu wanayoendelea kuipata inaendelea kuwa kumbusha kupigania nafasi.

“Kumekuwa na changamoto ya rushwa katika kupata hizi nafsi kikubwa nataka kuwasihi akina mama kujiamini kama wanaweza kumudu vyema kinyang’anyiri kama wanavyoweza kumudu kuelea familia basi hata hizo nafasi wanaweza kuzipata vilevile,”
Amesema Mungu ametoa kipaji kwa kina mama kikubwa watumie elimu yao na wasikubali kuingia kwenye suala la rushwa kwani ni adui wa haki.

“Wasiingie kwenye rushwa wanaweza wasipate nafasi leo, lakini wanapaswa kujua nafasi yao itakwepo wakati wote ,mwanamke anayejiamini na anauwezo anayonafasi kubwa,”amesema

Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, Esta Samanya amesema wanawake kupigania nafasi ya uongozi ni kitu kizuri na wanakuwa kwenye nafasi kubwa ya kuelimisha jamii.

“Wanawake wakiwa na madaraka wanakuwa na nguvu zaidi ya kutoka kwenda kutoa elimu kwa jamii na wanawake wengine wanaotakiwa kuingia kwenye vyombo vya maamuzi,”amesema
 
Hata hivyo alipinga kitendo cha baadhi ya watu kukalia kwa muda mrefu nafasi ya viti maalumu kama haki miliki yao kwenye baadhi ya vyama kwamba kinarudisha nyuma jitihada za kuwawezesha wanawake.

Alishauri kunapaswa kutengenezwa sheria ya vyama itakayosimamiwa na msajili wa vyama vya siasa na vyama na ieleweke katika Katiba ya nchi kwamba mtu akae kwenye nafasi hiyo kwa vipindi viwili ili na wengine wapate nafasi.