Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake watakiwa kuwekeza katika nishati ya umeme

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto  akitazama baadhi ya teknolojia za nishati katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TaWoED) na programu mpya zilizopo katika taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Muktasari:

  • Wanawake nchini wametakiwa kujiamini na kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme ili iweze kuendelea kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Dar es Salaam. Wanawake nchini wametakiwa kujiamini na kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme ili iweze kuendelea kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Meya wa jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto wakati akifungua kongamano lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake katika sekta ya Nishati Tanzania (TaWoED) na kukutanisha wanawake wahandisi na wanafunzi wa vyuo kwa lengo la kujadili fursa zilizopo katika sekta ya nishati.

Kumbilamoto alisema kuwa umefika wakati kwa wanawake wenye uwezo katika uwekezaji hususan kwenye uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme kujitokeza na kufanya biashara hiyo kwa ufanisi kwani uwezo wanao.

“Nataka niwahakikishie kuwa wanawake wanaweza na ndio maana hii leo tumeona wapo wengi waojihusisha na masuala ya uuzaji wa nishati ya umeme, kabla ya Rais hajatoa punguzo la umeme wa vijijini wa REA na mjini, solar ambayo inauzwa na kampuni za wanawake imekuwa ikisaidia sana jamii," alisema na kuongeza

"Wapo wanawake wanaotamani kupata tenda za serikali kuu au halmashauri ila vipo vikwazo hivyo nimewahakikishia sisi kama jiji tutaangali ni maeneo gani ambayo yanakwamisha ili tuyalaisishie na wao waingine katika ushindani hatimaye waanzishe kampuni zitakazosaidia kutoa ajira," alisema

Naye Mwenyekiti wa TaWoED, Gwaliwa Mashaka alisema wamezindua na kuleta kongamano hilo kwa lengo la kuwaleta pamoja wanawake waliokatika sekta ya nishati ili kuweza kujua fursa na tenda mbalimbali zinazotolewa kupitia sekta hiyo.

Alisema mtandao huo pia utakuwa na programu maalum kwa wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu waliosomea masuala ya uhandisi kupata elimu na kuwafundisha kwa vitendo ili waweze kuajirika na kuondokana na mtego wa kukosa kazi kwa kigezo kwamba hawana uzoefu.

Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya Nishati kutoka Kampuni ya Geni Energy Consulting Firm, Juliana Pallangyo amewataka wanawake ambao wapo kwenye sekta ya nishati ya umeme kufanya kazi kwa weledi, kujiamini na kutokata tamaa.

"Mimi nimekuwa katika sekta hii ya nishati zaidi ya miaka 40 na nikiwa kama Naibu Katibu Mkuu Nishati niliweza kusimamia ile timu ya kwanza ya maandalizi yote wa mradi wa Julius Nyerere ambao unaendelea vizuri na nilikuwa katika timu ile ya kuhakikisha bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka bandari ya Tanga Tanzania linapita hapa nchini, " alisema