Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapotoshaji bandari kushughulikiwa Tanga

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema Serikali mkoani kwake itawashughulikia wale watakaopita mkoani humo wakipotosha kuhusus mkataba wa uwekezaji wa kuiendelezaji wa bandari nchini.

Korogwe.  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema Serikali mkoani kwake itawashughulikia wale watakaopita mkoani humo wakipotosha kuhusu mkataba wa uwekezaji wa kuiendeleza bandari nchini.

Ametoa ahadi hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi mazoezi mjini hapa.

Amesema wanaoptosha kuhusu mkataba huo wamekuwa wakidai nchi imeuzwa kwa waarabu ili wananchi waweze kuwachukia waarabu, wakati Serikali imekuwa ikiingia mikataba bila kuwabagua wawekezaji kwa rangi wala utaifa wao.

"Nikuhakikishie Katibu Mkuu, wale wapotoshaji watakapokuja Tanga waje kwa heshima kama watakuja kivingine wajue tuta ‘deal’ nao kwa sababu wanadanganya kuwa hata bandari ya Tanga imeuzwa wakati wala haipo hata katika mkataba huo wa Dar es salaam" amesema Kindamba.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema mkataba wa uwekezeaji katika bandari ya Dar es salaam utaongeza mapato na kuinua uchumi wa Tanzania.

Chongolo yupo katika ziara Mkoani Tanga akiwa ameambatana na Naibu Waziri, Mwakibete, Steven Wasira na Mbunge wa ukonga jijini Dar es salaam, Jerry Slaa