Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasanii Orijino Komedi wahojiwa, washikiliwa polisi

Muktasari:

  • Wasanii hao, Lucas Muhuvile maarufu Joti, Alex John “Mac Reagan” na Isaya Gideon “Wakuvanga” wamehojiwa leo sambamba na meneja wa kundi hilo, Sekioni David.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Dar leo limewahoji wasanii wa Orijino Komedi makosa ya kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii mwenzao Emanuel Mgaya “Masanja”.

Wasanii hao, Lucas Muhuvile maarufu Joti, Alex John “Mac Reagan” na Isaya Gideon “Wakuvanga” wamehojiwa leo sambamba na meneja wa kundi hilo, Sekioni David.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Dar zinaeleza kuwa wasanii hao walikamatwa tangu jana jioni na kulala kituo cha Polisi hadi walipohojiwa juu ya tukio hilo.

Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinawaonesha wasanii hao wakiwa wamevalia sare zinazofanana na zile za Jeshi la Polisi wakiwa wanafanya gwaride, kama ishara ya kumpa heshima mwenzao, Emmanuel Mgaya “Masanja” aliyeachana na ukapera.