Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasiofahamika waiba vikombe nyumba ya watawa

Muktasari:

  • Mtu asiyefahamika ameingia nyumba ya watawa wa Shirika la Veronika lililopo Soweto, wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro na kuiba vikombe vya kuwekea komunyo (siborio).


Moshi. Mtu asiyefahamika ameingia nyumba ya watawa wa Shirika la Veronika lililopo Soweto, wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro na kuiba vikombe vya kuwekea komunyo (siborio).

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema kutokana na uzembe uliofanyika, wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo ya watawa ambaye hakutaka kutaja jina lake ili kujua ni nini kilichotokea.

Mtu huyo anadaiwa kuingia kwenye bomba kubwa la maji na kufanikiwa kuingia kwenye nyumba hiyo ya watawa usiku wa Agosti 15, mwaka huu na kuchukua vikombe vinne ambavyo vinatumika kuwekea komunyo.

“Tunamshikilia mtu mmoja ambaye ni mlizi wa nyumba ya masista na hapa inaonekana kuna uzembe ulifanyika, ndio maana tunamshikilia mlinzi kwa sababu hawakufunga mlango na huyo mtu alipitia na kupenya kwenye bomba na kuingia kwenye chumba ambacho kinahifadhi vikombe vya sakramenti (komunyo),” alisema na kuogeza:

“Tunamshikilia mlinzi kwa sababu ndio jukumu lake la kutoa taarifa maana baada ya tukio kutokea hakutoa taarifa mahali popote, kwa hiyo tunamshikilia na sasa tunaendelea na msako mkali wa kumtafuta aliyehusika na wizi huo,” alisema

“Baada ya tukio hili kuripotiwa tulifika kwenye hiyo nyumba ya watawa na kuna vikombe vya kuwekea sakramenti (komunyo) kama vinne hivi vilichukuliwa kwa hiyo tunaendelea kutafuta hawa waliohusika,” alisema na kuongeza kuwa wanafuatilia kujua vilikopelekwa vikombe hivyo, huku akiamini kuwa vitapatikana.