Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataalamu wa fiziolojia wakubaliana kuongeza tafiti

Muktasari:

  • Wataalamu wa fiziolojia (physiology) wakiwemo madaktari bingwa zaidi ya 100, kutoka mataifa 22 wapo nchini kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Afrika Mashariki wa taaluma hiyo unaolenga kuboresha na kuongeza utafiti katika magonjwa.

Dar es Salaam. Wataalamu wa fiziolojia (physiology) wakiwemo madaktari bingwa zaidi ya 100, kutoka mataifa 22 wapo nchini kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Afrika Mashariki wa taaluma hiyo unaolenga kuboresha na kuongeza utafiti katika magonjwa.

Wataalamu hao wamekutaja kuanzia jana Desemba Mosi kwa lengo la kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusiana na taaluma hiyo.

Fiziolojia ni fani ya kitabibu inahusiana na jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi katika hali ya kawaida na hali ya magonjwa.

Akifungua mkutano huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Profesa Appolinary Kamuhabwa, amesema taaluma hiyo inapaswa kuboreshwa ili kutatua changamoto za kiafya hasa wakati huu dunia inapopambana na magonjwa yasioambukiza kama vile kisukari, saratani na shinikizo la damu.

“Sisi Watanzania tunajivunia mkutano huu kufanyika hapa nchini na unashirikisha zaidi ya washiriki 200, kutoka katika bara ya Afrika, Amerika na Asia ambapo washiriki 100 kati ya hao wanahudhuria kwa njia ya mtandao,” alisema Profesa Kamuhabwa.

Amesema huo ni mkutano wa kwanza kufanyika nchini tangu wana fiziolojia hao waanzishe chama chao, ambapo watajadili na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha mafunzo, tafiti na huduma za afya kwa upande wa fiziolojia.

Profesa Kamuhabwa amesema fizioloji ni taaluma katika masuala ya mafunzo na matibabu kwa magonjwa ya binadamu.

“Utafiti wa magonjwa ukiwemo Ukimwi zinaendeela kufanyika na sisi Muhimbili ambacho ni chuo kikokwe katika utafiti na mafunzo kwa upande wa afya, tumefanya vizuri na baadhi ya miongozo na dawa mnazoziona chuo chetu kimetoa mchango wake vizuri,” amesema Profesa.

Kwa upande wake, Rais wa chama hicho cha Fiziolojia, Profesa Abdullatif Alagbonsi amesema mkutano huo utasaidia kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa pamoja na matibabu.

Awali, Profesa Emmanuel Balandya ni ambaye ni Naibu Kaimu Makamu Mkuu wa Muhas upande wa taaluma, amesema mkutano huo umekuja wakati muafa na utakuwa chachu ya kuendeleza familia hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Kama mnavyofahamu fiziolojia ni fani ya kitabibu inahusiana na jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi katika hali ya kawaida na hali ya magonjwa, hivyo wataalamu watajadili masuala ya utafiti na uchunguzi,” amesema Profesa Balandya.