Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania wakumbushwa kusaidiana

Nabii Mkuu Dk Moses GeorDavie (Katikati)

Muktasari:

  • Wamesema ni muhimu kujenga utamaduni wa kuchagua watu kupitia sanduku la kura ili kuleta amani na utulivu kwani viongozi watakaopatikana humo watakuwa ni wale waliokubaliwa na wengi.

Dodoma. Watanzania wenye sifa ya kupiga kura wameitwa kujitokeza siku ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, ikielezwa kufanya hivyo ni njia ya kupata viongozi wenye kibali cha Mungu.

Wito huo umetolewa leo Jumamosi Julai 5, 2025 na Nabii Mkuu, Dk Moses GeorDavie muda mfupi baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari wa heshima kwa masuala ya uongozi na maendeleo katika jamii ambayo amekabidhiwa na uongozi wa Association of Philosophical Doctors and Professors Tanzania (APDPT).

Kabla ya kutunukiwa shahada hiyo, Geordavie alikuwa na Shahada ya Uzamifu (PhD) aliyoipata kutoka Chuo cha American University.

GeorDavie ambaye ni kiongozi wa makanisa ya global Concert Churh (Ngurumo ya Upako) amesema bila kupiga kura haisaidii kuileta amani duniani.

Kiongozi huyo amesema upigaji wa kura ndiyo msingi katika Taifa lolote duniani kwani ni njia bora ya kuwapatia amani wananchi wao.

“Uchaguzi ni nguzo imara ya kujenga Taifa, ili tuwe na utulivu ni lazima watu wajitokeze kwenda kupiga kura ili viongozi watakaochaguliwa wakubalike kutokana na wingi wa kura walizopata,”amesema GeorDavie.


Nabii huyo amewataka wenye uwezo kujenga utamaduni wa kuwasaidia wahitaji kwa kuwa wapo wanaopoteza maisha kwa sababu ya kukosa kitu.

Amesisitiza kusaidiana siyo dhambi kwani kunachangia kupeleka tabasamu kwa wenye uhitaji na wakati mwingine huwaongezea hata siku za kuishi.

“Katika kipindi cha miaka mitatu mimi binafsi nimechangia katika jamii zaidi ya Sh3 bilioni ambazo zimepelekwa kusaidia yatima, wajane na watoto wanaoishi mitaani na zingine zilielekezwa katika miundombinu,” amesema.

Mwenyekiti wa jukwaa la Maridhiano na Amani, Alhaj Mussa Salim amesisitiza upendano na amani kwa Watanzania ili kulinda na kudumisha amani iliyopo sasa kwa faida ya leo na vizazi vijavyo.

Alhaj Mussa ametaja siri ya hayo yote ni kila mtu kuacha wivu kwani aliyepewa amepewa huku akisisitiza imani za watu kulindwa na kusimamiwa kwani, wote wanamwabudu Mungu kupitia imani yake.

Mwenyekiti wa APDPT, Profesa Rejoice Ndalima amesema umoja huo kwa kushirikiana na vyuo vingine wataendelea kutambua mchango wa watu waliofanya mambo makubwa kwa jamii ili kuwapa motisha na kufungua milango kwa wengine.

Profesa Ndalima amesema maisha ya Watanzania kwa sasa yanataka kusaidiana zaidi kwani hakuna mtu atakayetoka mbali mwenye huruma za ujomba ili aje kuwasaidia.

 “Lakini kingine niwaase viongozi wa dini, kuna makini na mambo mengi yanayotokea, ukiona upepo unapiga inama utulie, pakitulia nyanyuka na kupaza sauti bila kuchoka. Nasisitiza swala la kusaidiana kwa wenye uhitaji hasa wakati huu,” amesema Profesa Ndalima.