Watoto 2,300 wamebakwa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Muktasari:
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka 2016, matukio 1,765 yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi nchini.
Dodoma/Dar. Matukio ya ubakaji watoto nchini yameongezeka kutoka watoto 422 mwaka 2014, kufikia matukio 2,358 mwaka jana.
Hayo yalisemwa bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika inayofanyika leo.
Ummy amesema kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka 2016, matukio 1,765 yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi nchini.