Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto wanne wafariki wakioga kwenye dimbwi

Muktasari:

Watoto wanne wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye dimbwi wakati wakiogelea.

Sengerema. Watoto wanne wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye dimbwi wakati wakiogelea.

Kati yao, wawili ni wa familia moja wote kwa pamoja wakiwa wakazi wa kitongiji cha Mwambao Kijiji cha Chamabanda Kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amethibitisha kutokea tukio hilo akiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao wakati huu wa likizo kuepuka majanga hayo.

“Kwa sasa naelekea eneo la tukio kujioneo hali halisi, lakini wazazi wawe makini na watoto kipindi hiki cha likizo kuepuka majanga kama haya,”amesema Ngaga

Mwenyekiti wa Kitongiji cha Mwambao, Boniphace Mkama amesema inasadikika tukio hilo limetokea Septemba 12, 2023 saa 11 jioni.

Amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Matias Paul (8) anayesoma darasa la pili shule ya msingi Chamabanda,  John Thomas (8) mwanafunzi wa shule ya msingi Chamabanda anayesoma darasa pili, Majaliwa Festo (10) mwanafunzi wa shule ya msingi Chamabanda anayesoma darass la nne na Metod Paul (8) ambaye alikuwa hajaanza shule.

Amesema baada saa 2 usiku kufika bila watoto kuonekana kwenye  familia zao, majirani, baadhi ya ndugu na jamaa walianza kuwatafuta ndipo waliekea  barabara ya idara ya maji walipofika kwenye dimbwi waliona nguo za watoto hao zikiwa juu ndipo walipohisi wamezama.

Amesema baada ya kuona hivyo walipiga mwano wananchi walijaaa na kuanza kuwatafuta watoto ambapo walitumia zaidi ya saa mbili ndipo waliona na kuopoa miili ya watoto hao.

Mkazi wa Kitongiji cha Mwambao, Makiwa File amesema tukio hilo limetokea kwa mara ya kwanza eneo hilo.