Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto wawili wa familia moja wateketea kwa moto Moshi

Nyumba yenye vyumba vitatu ambayo imeteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watoto wawili katika Kijiji cha Shinga kata ya Uru Kusini, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea leo watoto hao wakiwa wamelala wakati baba yao alipoenda dukani kununua sigara.

Moshi. Watoto wawili ambao ni wa kike na kiume, wenye umri wa miaka miwili na nusu na mwingine miaka miwili na miezi minne katika Kijiji cha Shinga, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wameteketea kwa moto baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuungua.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo, Februari 28, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea leo watoto hao wakiwa wamelala wakati baba yao alipoenda dukani kununua sigara.

"Baba wa hawa watoto aliondoka muda mfupi kwenda kununua sigara dukani wakati anarudi akakutana na moshi mkubwa ukitoka ndani ya nyumba hiyo, ambapo watoto wote wawili walioteketea kwa moto," amesema Kamanda Maigwa.

Aidha, Kamanda Maigwa amesema chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.