Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 17 wapoteza maisha ajali ya basi, lori Kenya

Muktasari:

 Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu ambapo basi limegongana na lori wakati likijaribu kulipita gari dogo.

Kenya. Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya barabarani iliyohusisha basi pamoja na lori imefikia 17, huku majeruhi wakiwahishwa hospitali.

 Tovuti ya Taifa leo imeripoti kwamba ajali hiyo imetokea saa nane usiku wa kuamkia leo Jumatatu katika eneo la Othoo, Nyando katika Kaunti ya Kisumu.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba ajali hiyo imehusisha lori na basi la Super Metro lililokuwa likielekea Mombasa.

Inaelezwa kuwa basi hilo lilikuwa linajaribu kulipita gari dogo, ghafla likavaana na lori hilo lililokuwa limebeba mpunga, huku madereva wakidaiwa kufariki papo hapo.

“Tuliamshwa na sauti ya kishindo na tulipowahi eneo la ajali tulishuhudia vipande vya basi na lori vikiwa vimesambaa barabarani, amesema shuhuda James Onyango.

“Majeruhi walikuwa wakilia kutokana na maumivu ya majeraha waliopata,” amenukuliwa Onyango, mkazi wa eneo hilo.

Shuhuda mwingine Peter Otieno amesema walifanikiwa kuona miili 11 ukiwemo mwili wa mtoto wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa naibu Msimamizi wa Idara ya Afya Kaunti ya Kisumu, Ibrahim Wanyande amesema abiria 12 waliopata majeraha madogo wametibiwa na kuruhusiwa.

“Watu 15 wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga. Wawili wako mahututi,” amesema Wanyande.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Ahero, Grace Thuo ameliambia Taifa Leo kuwa miili 12 imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Ahero.

Kamanda Thuo amesema wanaendelea kufuatilia ili kujua idadi kamili ya abiria waliokuwa katika basi hilo wakati ajali hiyo ikitokea.