Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu nane wanaswa wakisafirisha mihadarati

Kamanda wa Pilisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo akionyesha vitu vilivyokamatwa mkoani humo ikiwamo dawa za kulevya.

Muktasari:

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelekezi kukamilika.

Tanga.  Jeshi la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelekezi kukamilika.

Hayo yalibanishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema hatua ya kukamatwa watuhumiwa hao inatokana na mafanikio ya operesheni na misako.

Misako hiyo imekuwa ikiendeshwa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali ambapo pia ilifanikiwa kuwakamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na biashara za uuzaji wa pombe haramu ya moshi na dawa hizo za kulevya za viwandani.

Alizitaja dawa hizo za kulevya ambazo zimekamatwa kuwa ni kilo 300.08 za mirungi, gramu 4 za Heroine, kilo 87 za bangi na pombe ya moshi (gongo) lita 180.

Wakati huo huo Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mali za wizi zikiwamo televisheni 13, vingamuzi mbili, deki ya DVD moja, laptop mbili, simu za mikononi 11 na pikipiki mbili kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi ambao waliibiwa vitu hivyo wafike kituo cha Polisi Chumbageni ili waweze kutambua mali zao.

Kamanda Jongo amesema silaha za kienyeji aina ya magobole 23 yalimatwa katika wilaya za Pangani na Kilindi mkoani humo ambapo watuhumiwa wamekiri kujihusisha na uwindaji haramu.