Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watuhumiwa 12 kesi ya uhujumu uchumi wapindishwa kizimbani Masasi

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao  baadhi ni viongozi na watendaji wa Kijiji cha Chigugu, wakikabiliwa na makosa 27 ya uhujumu uchumi.

Mtwara. Mahakama ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imewapandisha kizimbani watuhumiwa 12 wanaokabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi lenye jumla ya makosa 27 yanayohusiana na rushwa na kughushi nyaraka.

Watuhumiwa hao, ambao baadhi yao ni viongozi na watendaji wa Kijiji cha Chigugu wilayani Masasi, walifikishwa mahakamani leo Juni 10, 2026 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Rehema Iddy kwa ajili ya kusomewa mashtaka hayo.

Waliopandishwa kizimbani ni Merchior Mchopa, Jackson Ngombe, Michael Millanzi, Francis Chilumba, Mohamed Katopola, Hamis Namkutwanga, Husna Mohamed, Bibie Chivalama, Mbaraka Namkutwanga, Hamis Kalanje, Hamza Rashid na Ismail Ngunga.

Akisoma mashtaka, Hakimu Iddy amesema kesi namba 12683/2026 inahusu tuhuma za udanganyifu katika utekelezaji wa mradi wa bomba la maji kutoka Ndanda-Mbwinji kwenda Masasi mwaka 2016.

Amesema watuhumiwa wanadaiwa kushiriki katika vitendo vilivyosababisha wananchi saba kulipwa zaidi ya Sh6 milioni isivyo halali kupitia mradi huo. Ilidaiwa kuwa mwaka 2018 walihusika katika udanganyifu wa malipo ya fidia yaliyokuwa yakitolewa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Masasi (Manawasa).

Upande wa mashtaka umedai malipo hayo yalifanyika kwa kutumia nyaraka zenye taarifa zisizo sahihi, hali iliyoisababishia Serikali hasara ya fedha. Pia ilielezwa kuwa uchunguzi umebaini viashiria vya matumizi ya nyaraka za kughushi ili kuwezesha malipo hayo kufanyika kinyume cha taratibu.

Watuhumiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili mara baada ya kusomewa mahakamani.

Wakili wa Serikali, Charles Mtungila, aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo akieleza kuwa uchunguzi wa baadhi ya vipengele bado unaendelea ili kukamilisha maandalizi ya ushahidi, ambapo kesi hiyo hadi Juni 22, 2026 kwa hatua nyingine za kisheria.