Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watumishi saba wa Serikali kuchukuliwa hatua

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa.

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ameagiza watumishi saba wachukuliwe hatua.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ameagiza watumishi saba wa Halmashauri ya Liwale mkoani Lindi, wachukuliwe hatua.

 Agizo hilo, amelitoa leo, Septemba 18, 2023 kupitia barua ya Mchengerwa iliyotiwa saini na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Ntenghenjwa Hosseah, ikimtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sospeter Mtwale awachukulie hatua.

Kulingana na barua hiyo iliyotolewa leo, watumishi watakaochukuliwa hatua hizo ni Sisty Nyau (Kaimu Mhandisi wa Wilaya), Damas Mumwi (Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika) na Vinsent Moyo (Mkuu wa Idara ya Ugavi na Manunuzi).

Wengine ni Mohamedi Songolo (Mkuu wa Idara ya Tehama), Sadick Khatibu (Katibu wa Afya) na Tunu Mtamaha (Ofisa Ugavi na Ununuzi aliyehamishiwa halmashauri ya Wilaya ya Kilwa).

Barua hiyo imetaja sababu za hatua hizo ni watumishi hao kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo, kuzorotesha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za halmashauri hiyo.

Mbali na hatua dhidi ya watumishi hao, Mchengerwa ameelekeza kusimamishwa kazi, badala ya kuhamishwa maofisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhirifu hadi mashauri yao yatakapokamilika.

“Ofisa yeyote mwenye kesi ya uhujumu uchumi au ubadhirifu wakati kesi yake ikiendelea ataendelea kuchunguza mienendo yake na hukumu yake ikitoka hatopewa tena jukumu la ukuu wa Idara au Kitengo,” amesema.