Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wauza chakula wafurahia fursa, walia na vishoka

Muktasari:

  • Wauza chakula na vinywaji ni kundi mojawapo lililopata fursa katika maonyesho ya wajasiriamali yanayotamatika leo jijini hapa kwa nyakati tofauti maelezea neema waliyoipata ndani ya siku hizo huku wakilia na uwepo wa wauzaji wasio na mialiko maarufu kwa jina la vishoka.

Dar es Salaam. Kundi la wafanyabiashara wa chakula na vinywaji katika maonyesho ya wajasiriamali yaliyofanyika kwa siku tatu kuanza Septemba 11 hadi 13, jijini hapa wameelezea namna walivyonufaika na maonyesho hayo sambamba na kutoa kero walizokumbana nazo.

 Wakizungumza na Mwananchi leo Septemba 13 katika viwanja vya Mnazimmoja wamesema wamepata nafasi ya kuuza chakula na vinywaji lakini changamoto waliyokutana nayo ni utaratibu usioridhisha ikiwemo kutokuwa na vitambulisho.

Mama lishe kutoka banda la Lishe Group kutoka Soko la Samaki Feri, Batreti Malemula, amesema wanashukuru Taasisi ya CRDB benki Foundation na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kupata fursa ya kuuza chakula lakini anaomba uwepo wa vitambulisho.

Batreti amesema kuna wauzaji waliovamia bila kupewa mualiko wa Ofisa maendeleo wanaowaharibia biashara.

"Wenzetu wanauza bei juu, unakuta soda tunauza Sh800 lakini wao wanauza Sh1, 000 na watu hawajui unakuta wananunua, supu ya samaki tunauza Sh2, 500 wao wanauza hadi Sh5, 000 unakuta wateja wanakimbia," amesema Batreti.

Ameomba wapewe vitambulisho maalumu ili watambulike waweze kufanya biashara zaidi.

Maneno ya Batreti yanaendana na Leyla Kawagalise muuzaji wa chakula ambaye amesema moja ya faida aliyoipata amejifunza kutengeneza juisi ya matunda ambayo itamuongezea chachu katika biashara yake ya chakula.

Akizungumzia changamoto amesema utaratibu unapaswa uangaliwe upya ili waweze kufanya biashara hata katika maonyesho yajayo.

Amesema anauomba uongozi usimamie wauzaji wasiofuata utaratibu.

Aidha ameshukuru waandaaji wa maonyesho hayo yanayotamatika leo, pamoja na kuomba muda kuongezwa zaidi lakini pia iwepo siku ya wajasiriamali.

Mama lishe mwingne ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema katika siku tatu hizo hakukuwa na utaratibu wa kudhibiti wamachinga na kushauri uzingatiaji wa idadi yao kama wauz chakula.

"Lazima kuwe na utaratibu wa kudhibiti idadi ya wafanyabiashara kuendana na idadi ya watu waliopo, tuko wengi kila mtu anauza. Nashauri kungekuwa na idadi kamili ya waizaji wanaohitajika," amesema.

Amegusia pia uwepo wa viongozi au watu mashuhuri kuleta hamasa wakati wa maonyesho hayo ili kuvutia watu zaidi waweze kufika viwanja hivyo.

Ameongeza kuwa anashukuru kwakua wamekuwepo viwanja hivyo bure bila malipo ya ulinzi wala vibanda.

Alipotafutwa na Mwananchi, Ofisa Maendeleo Wilaya ya Ilala Fransisca Makoye ameahidi kuyafanyia kazi.

Amesema katika maonyesho yajayo yatakuwa na taratibu zote kama maoni yaliyotolewa.

"Tumepokea hayo maoni nakatika maonyesho yajayo tunamini tutafuata kila kilichotolewa maoni," amesema Fransisca.