Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili mbaroni kutumia jina la Mo Dewji kutapeli

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga akionyesha sehemu ya nyaraka za kugushi zilizokuwa zikitukiwa na watuhumiwa wawili wanaoshikiliwa kutoa kutapeli kutoa mikopo isiyo na riba. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi limethibitisha kushikiliwa kwa watu hao ambao mbali na kutapeli wamepatikana na nyaraka mbalimbali   za kugushi zikionyesha uendeshaji halali wa kutoa mikopo kwa riba nafuu.

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana wawili kwa tuhuma za kufanya udanganyifu na kutapeli mamilioni ya fedha za wananchi kwa kutumia  jina la taasisi ya mfanyabishara maarufu Mo Dewji Foundation kutoa mikopo ya riba nafuu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 23, 2023, watuhumiwa hao walikamatwa jana Oktoba 22 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ya Alta's iliyopo mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya wakiwa na nyaraka mbalimbali za mikopo ambazo zikionyesha picha ya mfanyabiashara Mo Dewji.

Kamanda Kuzaga amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Sarael Geshon (19) na Christian Erasto (21) wote wakazi wa Kijiji cha Chakakazi Wilaya ya Mbeya na walipohojiwa wamekiri kuhusika na matukio kadhaa ya kufanya utapeli.

“Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni kufuatia taarifa za wananchi kulalamikia kutapeliwa na ndipo, Polisi walipoweka mitego na kufanikiwa kuwanasa huku wakiwa vitu mbalimbali vya kugushi vinavyoonyesha uhalali wa kuendesha Taasisi ya Mo Dewji Foundation,”amesema.

Kuzaga amesema baada ya Polisi kufanya upekuzi wamebainika kuwepo na Tin namba za TRA, Nida, leseni za biashara zilizosajiliwa na Brela kwa jina la Mo Dewji Foundation ambapo zinaonyesha kutoa mikopo kwa riba nafuu.

Ametaja vitu vingine kuwa ni simu za mkononi aina ya smart phone sita, simu ndogo tatu  laini za mtandao wa vodacom 10 tigo mbili na Airtel tatu  zenye usajili wa majina tofauti tofauti ambazo zilitumika kuwashawishi na kuwaibia watu ambao wanahitaji  mikopo sambamba na kusambaza  machapisho mbalimbali.

Katika tukio la pili mkazi wa Nsalaga mkoani hapa, Joshua William (19) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kupatikana na pikipiki ya matairi matatu (Bajaji) ya wizi.

Kamanda Kuzaga amesema mtuhumiwa amekatwa Oktoba 22, 2023 katika kituo cha mabasi yaendayo mji Tunduma iliyopo eneo la Mbalizi akiwa kwenye  harakati ya kuisafirisha kupeleka Mkoa wa Songwe.

“Mtuhumiwa amekiri kuhusiana na tukio la wizi lililotokea Oktoba 21, mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku katika Kijiji cha Shigamba nje ya nyumba ya mmiliki wa bajaji hiyo aliyetajwa kwa jina la Emmanuel Obimsonge (38).

Kamanda Kuzaga amewataka wananchi walio tapeliwa na watuhumiwa hao kufika Kituo cha Polisi Mbalizi sambamba na nyaraka ambazo walipatiwa kwa ajili ya kupewa mikopo ili walisaidie ushahidi na watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

Akizungunza na Mwananchi mmiliki wa bajaji hiyo, Emmanuel amesema siku ya tukio alikodiwa na watu watatu akiwepo mtuhumiwa na wanawake wawili ambao walimtaka awapelekea katika Night Club  ya Mbeya Pazuri.

“Ingawa roho ilisita lakini niliwaomba niende nyumbani kuchukua koti na kumuaga mke wangu kwani ilikuwa ni usiku na kwamba mara baada ya kufika na  kuingia ndani ndipo walitumia  mwanya wa kuiba na kutoweka nayo.

“Nilitoa taarifa Polisi nashukuru kwa ushirikiano mkubwa wa kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na bajaji hiyo ikiwa salama pasipo kufanyika uharifu,”amesema.

Mkazi wa Mji wa Mbalizi, Joyce Mwakilima amesema kuwa  kumekuwepo na matukio mbalimbali ya kiharifu yakihusisha wizi wa pikipiki na kuomba Jeshi la Polisi kufanya doria za mara kwa mara ili kukabiliana nayo.