Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazazi, walezi kuwa walinzi ulimwengu kidijitali

Watoto wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika, jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, wazazi watakiwa kusimamia malezi na kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mitandaoni, hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kidigitali.

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, wazazi watakiwa kusimamia malezi na kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mitandaoni, hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kidijitali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi na wadau mbalimbali, wamewataka wazazi kuhusika kikamilifu katika malezi ya watoto na hivyo kuwa msaada na ulinzi dhidi ya mambo yafanyikayo mitandaoni.

Akizungumza jijini hapa leo Juni 16, 2023; Katibu Tawala Wilaya ya Ilala (DAS) Charangwa Selemani, amesisitiza wazazi kutokuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto.

DAS huyo amesma wazazi huchangia bila wao kujua na hasa wanaporuhusu matumizi ya simu kwa watoto pindi wanapokuwa hawataki usumbufu.

Kiongozi huyo ametoa mfano kwa kusema: "Mzazi akiona vurugu zimezidi anamkabidhi mtoto simu achezee, ama kuangalia runinga, wakati kuna vipindi ambavyo haviendani na maadili ikiwepo mambo ya ushoga."

Aidha, amewataka wazazi kutowaamini wageni wanaowakaribisha nyumbani kulala na watoto kwani matukio mengi ya ubakaji na ulawiti yamekuwa yakisababishwa na watu wa karibu.

Pia amewataka wazazi kuwa karibu na watoto ili kuwaelezea changamoto wanazokutana nazo ikiwepo vitisho vya kuuawa pindi wanapofanyiwa vitendo vya kikatili.

"Wanaume wametoka katika uhalisia wa ubaba na kusababisha matatizo kwa watoto, endapo watarudi katika misingi ya dini watoto wetu hawawezi kuharibikiwa kwa kuamini yupo katika mikono salama," amesema Charangwa.

Naye Mratibu wa mradi wa kuimarisha familia (Sos children's village) Kennedy Mashema, amesema mradi wao umesaidia watoto kupitia vikundi vidogo vidogo ikiwemo Vikoba.

Amesema kumekuwa na matukio mengi ambayo yanawaathiri watoto kisaikolojia kutokana na hali ya kiuchumi kwa familia ikiwemo kukosa haki zao za msingi.

Kwa upande mwingine Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimeitaka jamii kuongeza ulinzi kwa watoto kwa kuwakinga na vitendo vya ukatili.

Vitendo hivyo kwa mujibu wa Tamwa ni ukatili wa mitandaoni, mimba za utotoni, ndoa za utotoni, ulawiti, ubakaji, ukeketaji, unyanyapaa na ajira za watoto.

Mkurugenzi wa Tamwa Dk Rose Reuben amesema ni  jukumu la wazazi na walezi kuwafundisha watoto matumizi sahihi ya mitandao ya kijami.

“Katika hali isiyo yakawaida, nyumbani, shuleni, barabarani pamoja na nyumba za ibada zimekuwa ni sehemu zinazoripotiwa kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto," amesema.

Dk Rose ameonyesha kutoridhishwa na ukweli kwamba wengi wanaofanya matukio dhidi ya watoto ni wale walipewa jukumu la kumlinda.

Walinzi hawa wa mtoto ni pamoja na wazazi, walimu, walezi, ndugu pamoja na majirani.

“Ili kumlinda mtoto wa afrika Tamwa tunaomba ushirikiano wa wadau wote wakiwemo wazazi, walezi, wanasheria, na Serikali kwa ujumla," amesam na kuongeza;

"Pia wadau wa maendeleo, tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto wetu ni wa uhakika na endelevu.”