Wenje acharuka ongezeko la migogoro nchini

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje.

What you need to know:

  • Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje amesema wingi wa migogoro nchini ni ushahidi kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kuongoza nchini.

Bariadi. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje amesema wingi wa migogoro nchini ni ushahidi kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kuongoza nchini.Wenje ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika leo March 16, 2023 mjini Bariadi mkoani Simiyu ambapo amesema katika mikutano yote ambayo imefanyika wamekuwa wakikutana na migogoro ya aina mbalimbali."Tumekuja kukumbusha tena kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi, tuna mwezi mzima tupo kwenye ziara ya kuzungumza na Watanzania kila sehemu tukienda wananchi wanamigogoro kuna matatizo," amesema Wenje.Amesema kuimarika migogoro hiyo inasababishwa na uongozi uliopo madarakani ambapo haiwezekani mtendaji ambaye hajasoma aongoze wasomi na wafanikiwe kiutendaji.Ambapo ametolea mfano nafasi ya uongozi wa kamati za ulinzi na usalama katika wilaya kuongozwa na watu wasiokuwa na maarifa katika uongozi hivyo haiwezi kumaliza kero za uongozi.Aidha, amesema Serikali imekuwa na matumizi mabaya ya kodi za wananchi katika kujiendesha ambapo imewekeza katika kutengeneza mabango ya kusifia badala ya kutoa kipaumbele katika maendeleo ya wananchi."Hiyo siyo kazi ya kodi za wananchi, hakuna kiongozi atakayetokana na Chadema atayeendekeza matumizi ya hivyo hatutakubali," amesema Wenje.Sambamba na hayo amesema kumekuwa na bajeti kubwa katika matukio ya kiserikali yasiyokuwa na tija ambapo amesema iwapo chama hicho kitachukua madaraka hayatakuwepo.