Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizara yarekebisha kanuni ya madini Tanzanite

Wizara yarekebisha kanuni ya madini Tanzanite

Muktasari:

  • Wizara ya Madini imetimiza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kurekebisha kanuni ya madini ya Tanzanite kununuliwa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, sehemu pekee ambayo yanayopatikana duniani.

Mirerani. Wizara ya Madini imetimiza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kurekebisha kanuni ya madini ya Tanzanite kununuliwa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, sehemu pekee ambayo yanayopatikana duniani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akizungumza na Mwananchi Digital mji mdogo wa Mirerani, leo Jumamosi Julai 10, 2021 amesema kanuni za kuhakikisha madini ya Tanzanite yanauzwa Mirerani pekee zimekamilika.

Profesa Msanjila amesema kanuni hizo zimeshaandikwa na kutangazwa katika  gazeti la Serikali Julai 9, 2021  na zimeanza kutumika rasmi.

Amesema wanunuzi na wauzaji wenye leseni ya kununua madini hayo wameshapatiwa taarifa juu ya kuanza kutumika kwa kanuni hizo za madini ya Tanzanite kuuzwa mji mdogo wa Mirerani.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Caroline Mthapula amesema soko la kununulia madini hayo ya Tanzanite limeandaliwa mji mdogo wa Mirerani.

"Tumeshawaambia wafanyabiashara hao kuwa ununuzi ufanyike Mirerani ila ukataji na kuongeza thamani ufanyike popote ila rasmi kuanzia Oktoba 15 ikifika shughuli zote kufanyika ni Mirerani," amesema Profesa Msanjila.

Mthapula amesema eneo la mamlaka ya kusafirisha bidhaa nje (EPZA) limeanza kugawiwa kwa wanunuzi hao wa madini ili ujenzi wa ofisi uanze mara moja.