Zijue athari za woga kabla ya tendo la ndoa

Woga kabla ya tendo la ndoa ni tatizo linaloweza kuwatokea wanaume katika kipindi cha maisha yao na kuwasababishia kushindwa au kushiriki chini ya kiwango tendo la ndoa na wenza wao.

Ni tatizo linalompata mtu mara kwa mara na linaweza kuwa chanzo cha kupata tatizo la kuwahi kufika mshindo na kushindwa kuendelea mizunguko mingine au kukosa hamu ya tendo.

Tatizo hili linapomkabili mwanaume linaweza kuwa chanzo cha kuvunjika uhusiano au kuleta mifarakano katika mahusiano yao.

Mwanaume anaweza akaonekana mtulivu na anayeongea kuliko mwanamke lakini ndani ya mioyo yao huwa hofu hali inayomfanya kuwa mwoga hasa nyakati za matayarisho kabla ya tendo.

Yafuatayo ni mambo yanayompa hofu mwanaume na kumfanya kuwa mwoga.

Hofu ya kuwa hanithi (Impotence) ndiyo tatizo linaloongoza kuwafanya wanaume wapate woga wa kujamiana na wenza wao.

Nchini India, gazeti maarufu la Times India liliwahi kuripoti kuwa karibu asilimia 90 ya wanaume wenye tatizo la kushindwa kusimika husababishwa na matatizo ya kisaikolojia na asilimia 10 huwa ni ya kibaiologia.

Hofu ya maumbile madogo ya kiume ni mojawapo ya tatizo linachangia woga, wanaume kujihisi kuwa ana maumbile madogo na kumfanya kuwa na dhana kuwa atashindwa kukidhi hisia za kimwili za mwenza wake.

Wanaume wanashindwa kufahamu kuwa umbile dogo si chanzo cha kushindwa kumridhisha mwenza. Mwanamke anaweza akaridhishwa na kufika keleleni hata kwa mwanaume mwenye saizi ya kidole cha mtu mzima.

Hofu ya tatu ni tatizo la kuwahi kufika mshindo kabla ya kumridhisha mwenza, hili ni tatizo linalomweka mwanaume katika mawazo na kumfanya kuwa mwoga kushiriki tendo akihisi kuaibika kwakutomridhisha mwenza. Baadhi ya wanaume huweza kujihisi hawako kawaida wanapojilinganisha na wanaume wengine, anaposikia wenzake wanapojisifu kwa maumbile makubwa. Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu.