Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zitto aelezea maana ya ‘Shusha tanga, pandisha tanga’

Muktasari:

Waliokuwa viongozi mbalimbali wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwamo Maalim Seif Sharif Hamad wamehamia chama cha ACT-Wazalendo, hatua hiyo imekwenda sambamba na kuanzishwa kwa msemo ’Shusha tanga, pandisha tanga.’  Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ameuelezea una maanisha nini msemo huo.


Dar es Salaam. Kumekuwapo na misemo mingi katika siasa ambayo imekuwa ikitumiwa na wanasiasa katika vipindi fulani.

Miongoni mwa misemo ni ule ambao Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliwahi kusema kwamba endapo atafanikiwa kuingia pale magogoni katika jumba jeupe, basi yeye itakuwa ‘Kazi na bata’.

Msemo huo ulipokewa kwa hisia tofauti. Wapo waliopongeza na wengine kusema utawezekanaje iwe kazi na bata. Hilo likapita.

Sasa umeingia mwingine. Huu wa sasa ambao umekuja baada ya vigogo waliokuwa Chama cha Wananchi (CUF) akiwamo aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kutimkia ACT-Wazalendo umekuwa ukitumiwa wa ‘pandisha tanga shusha tanga’.

Unaweza kujiuliza, huu msemo una maana gani, kwa nini ‘shusha tanga na pandisha tanga?

Mwananchi limezungumza na Zitto kuhusu huo msemo amesema, “Kwenye jamii za bahari au ziwa maboti huwa na Tanga.”

“Tanga ni kitambaa kikubwa cha kusukuma majahazi kwa upepo. Tanga likiharibika unalishusha unapandisha tanga jipya.”

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini anasema, “Shusha tanga (shusha CUF) pandisha tanga (pandisha ACT-Wazalendo). Safari iendelee.”

Katika mizania hiyo ya ‘shusha tanga na pandisha tanga’, kesho ngome ya vijana Taifa ya ACT Wazalendo itawapokea waliokuwa viongozi wa kitaifa wa baraza la vijana CUF (JUVICUF).

Shughuli  hiyo itafanyika makao makuu ya chama hicho Kijitonyama jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi.